Tofauti ya lugha kwenye bar baina ya zama zile na zama hizi

Tofauti ya lugha kwenye bar baina ya zama zile na zama hizi

Zamani ni mwendo wa kreti chini ya meza kisha madem wanakuja wenyewe

Umenikumbusha mbali sana...hehehe
Kuna kipindi watu walikua na mazoea ya kumfuata waiter kisiri na kumuomba aletee kila mmoja chupa kumi kumi halafu anamlipa huko huko, yaani wadau wanaona chupa zinakuja na kujaza meza yote, ushindwe mwenyewe.
 
Lugha maarufu enzi zileeee.....;

1. Lete Tulivyokaa

2. Muongeze 5 huyo

3. Mbona bia haziendi?

4. Usiulize, wee Ongeza tu

5. Mbona jikoni hawatusikilizi??

6. Aah,tunahudumiwa na dume?

7. Nimesema Mbuzi mzima!!

8. Wee hizi ni kilo 5 kweli?

9. Kuna watu wanabusu bia!

10. Hamishia opener hapa hapa?

Zama hizi sasaaa.....
1. Waruke wote, sijaja nao mimi

2. Mmh, kaongeza nyingine?

3. Bia zenu bei mbaya zaidi ya jirani yenu?

4. dada, uliza kwanza hata kabla ya kuleta toothpiki

5. Tumekula majumbani kwetu

6. Nitanunulia kaunta mwenyewe

7. Mna kongoro?

8. Lete supu tu bila finyango kwani shingap?

9. Siku hizi inashauriwa bia 2 tu kwa afya

10. Hebu toa mavituvitu yenu hapa yanatuzingua

11. Nilitee bili ya bia nilizokuagiza mimi nyingine sizijui...

[emoji23][emoji23][emoji23]🕺🏼🕺🏼🕺🏼
Na Kenya hali iko hivyo? Nilidhani Tz tu
 
pia wanakua na hasira sana ukijichanganya unaweza kula chupa za kichwa.
 
Back
Top Bottom