Tofauti ya matumizi ya social media kati ya wazungu na watanzania

Tofauti ya matumizi ya social media kati ya wazungu na watanzania

Hao wamarekani wanavyochangia ndiyo vile watu wa Dar wanavyochangia mada...

Hao wakibongo wanavyochangia ndiyo vile watu wa miakoni nje ya Dar wanavyochangia mada...

Akili za kuambiwa...



Cc: mahondaw
Smart911 hivi Mahondaw ni mkeo?,hawala?dada?au ndugu?.Samahani nimetoka nje ya mada...maana swali hili huwezi kulifungulia sledi...inabidi kuulizamo mumo kwa mumo!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
TOFAUTI YA UCHANGIAJI WA MADA KTK FACEBOOK, KATI YA MAREKANI NA BONGO:

Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0710808312. Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

RAMESH MATUKUTUKU: Je, una tatizo la kuwahi kileleni, upungufu wa nguvu za kiume? Inbox me na tatzo lako litaisha ndani ya wiki moja ujenge heshima

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..

MTUMISHI: Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MAC MUGA: Tengeneza mpaka milioni mbili ndani ya wiki moja tu bila kuathiri kazi zako. Kwa maelezo zaidi nitafute 07356

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...

C&p
 
SIKU HIZI SEHEMU ZA KUTANGAZIA BIASHARA NI KWENYE POST ZA WATU DAAH
 
Ila wale Wanao comment kwenye ukurasa wa EATV nafikiri wengi ni under 25, maana akili zao za kitoto sana, halafu mambo mengi yanayoendelea duniani hawayajui kabisa
Hawa jamaa huwa wananifurahisha sana comment zao ni comedy aisee
 
Ukweli mtupu[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji872][emoji872]
 
Hahahahaha nadhani kwa Africa wanaigeria wanaongoza yaani mpaka hua wanatimuliwa kwenye forums/groups zingine,
wapo negative minded sana, wana mihemko, wanajifanya wanamjua sana Yesu, wanaweza wakamsimanga mtu mpaka akazimia.
Lol..wanaigeria wanashikilia namba moja kwa negativity kwenye social media aisee na kile kingereza chao sasa...nchi ninayoikubali linapokuja swala LA kujadili issues kwenye social networks ni kenya.
 
Huwa natafuta forums za kuwapata sijazijua bado zaidi ya BBC focus on Africa anakotangaza mnaija mwenzao Okwoche
Wanayo forum yao kubwa sana, nafikiri ndio forum kubwa kwa Africa inaitwa Nairaland forum, Tatizo viingereza vyao vitakushinda utasikia mara Oga, na, chop, don na kadhalika
 
Lol..wanaigeria wanashikilia namba moja kwa negativity kwenye social media aisee na kile kingereza chao sasa...nchi ninayoikubali linapokuja swala LA kujadili issues kwenye social networks ni kenya.
Yes, Kenyans wapo vizuri sana na South Africans.
 
Kila mtu ana mawazo yako. Lakin pale kwenye kumshaur mtu katika njia sahihi ndo hawana . Wanaona kuwa mpaka ampende huyo binamu maana yake alisha mtamani toka mda na sio siko hiyo tuu.
 
Back
Top Bottom