Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Habari wana intelligence.
Mwaka 2006 nikiwa darasa la 4 shule ya msingi huko kijijini kwetu, nikiwa nimelala usiku wa manane niliota nikiwa shule kama kawaida, kwenda na kurudi kama ilivyo haya maisha ya kawaida.
Nikahitimu shule ya msingi na kuanza kidato cha kwanza, cha pili, cha tatu na cha nne hatimae nikamaliza.
Nikakaa nyumbani nikiendelea na shughuli zingine wakati nasubiria matokeo ya kidato cha nne ghafla nikashtuka na kujikuta nipo kitandani.
Kule ndotoni nikiwa darasa la 6 nilivunjika mkono wakati nacheza mpira, nikakaa nyumbani kama mwezi na nusu na mkono ulipopona ulibaki na ukilema kidogo.
Pia kuna changamoto nyingi nilizipitia ambazo zilikuwa za kawaida, kama kutoroka shule, kuwakera wazazi wangu nk;.
Sasa niliposhtuka nilijiona hovyo sana kwa kujikuta nipo kitandani na inatakiwa kukikucha tu nijiandae niwahi shule ambayo nilikuwa darasa la 4 wakati mimi nilikuwa nasubiria matokeo ya kidato cha nne ndotoni ambayo niliyasotea kama ilivyo kawaida.
Furaha iliyonifariji kidogo ni kujikuta mkono sio kilema tena.
Kumbuka ile ajali ya kwenye mpira ndotoni ambayo iliniacha kilema sasa nilipoamka na kujikuta mzima kidogo ndio ilinifariji maana ukilema wangu nilikuwa nimeshauzoea kule ndotoni.
Sasa kule kuamka kukanipa kujiuliza maswali mengi ambayo hayana majibu.
Kama inakuakuaje nimeishi ndotoni kwa miaka mingi namna hiyo ilihali hii ndoto nimeiota ndani ya kama nusu saa tu au chini yake.
Na vipi haya maisha ya kawaida... Kuna siku labda nimelala kwenye ulimwengu fulani nikaingia kwenye ndoto ambayo ndio haya maisha niliyopo au.
Unaweza kulala mgonjwa na ukaamkia ndotoni ukiwa mzima ilihali muda utakapoamka utajikuta na ugonjwa wako.
Au Unalala mzima unaamkia ndotoni na matatizo kibao hata yasiyoelezeka au pengine kufa kabisa. Lakini ukiamka tu unajikuta na uzima wako.
Au Unalala na hali fulani na unaamkia ndotoni na hiyohiyo hali kama nilivyolala mimi, lakini ukiamka utajikuta pale ulipoachia.
Kama uliachia hatua tatu na ukaingia ndotoni ukaongeza nyingine tatu zikawa sita, utakapoamka utajikuta pale kwenye tatu uliyoacha.
Sasa nauliza tu kwamba, Haya maisha tunayoishi kuna uwezekano yakawa ni ndoto?
Maana yale ya ndotoni hayana utofauti na haya.
Je? Mwili tunaotumia ni huu huu au kuna miili mingine kila copy tunayochukua?
Unaweza ukajitahidi kufanya jambo fulani la maana ghafla ukajikuta ulikuwa unaota.
Naombeni mnisaidie kufafanua hili maana kila siku nadhani naota tu. Na kweli vingine saa nyingine nasema aah! Hii ndoto tu.
Na ghafla inakuwa ndoto kweli.
Apollo Kiranga Jimena Rakims na wengine weengi niliowasahau.
Karibuni

Last edited by a moderator: