Bennie 369
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 713
- 534
Ndio naendelea kujitajidi kwenye Maditation, na kwa sasa nimeona matokeo kidogo
Afu ludovick we mtata sana... .. .ulisema utaleta mrejesho hadi leo kimya 🙂
Cc; Jimena
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio naendelea kujitajidi kwenye Maditation, na kwa sasa nimeona matokeo kidogo
Jimena we kila siku ni kuempty mind tuuuu??? how abt focus????.
hence kuempty mind tuuu hukufanya u relax tu nakufanya body & mind kuwa katika hali ya kawaida
Well, sijasoma tangu mwanzo wa thread mpaka hapa mlipofika coz kuna wakati muda unakuwa hafifu kiasi.
Ila pia naweza kusema pengine ntakachojibu hapa chaweza kuwa kimeshasemwa ila tu ni kwa kuwa nimeitwa, basi mara nyingi hupenda kuitikia wito pale ninapoitwa.
Mi sina hakika kama ntaelekeza jibu langu kama lilivyouliza swali la mleta mada au sina hakika pia kama ntajibu tofauti sijui ni kitu gani ntakachoandika ila kifupi ni kuwa, swali la mleta mada linaweza kuwa na jibu rahisi tu tofauti na matarajio yake alivyotaka kujibiwa kwa maana gani ?, ndoto mtu huota usingizini na akiwa amelala na maisha ya kawaida ni maisha au hali inayomtokea mtu akiwa macho.
HIYO NDIYO TOFAUTI YA KATI YA NDOTO NA MAISHA YA KAWAIDA. NATUMAI NTAKUWA NIMEMJIBU MLETA MADA NDUGU aretasludovick.
LABDA TU KAMA KUTAKUWA NA SUALI JINGINEWE. SHUKRAN.
Kuna tofauti kati ya ndoto na maisha ya kawaida lakini pia kuna ufanano kati ya ndoto na maisha ya kawaida.
Maisha ni mazingaombwe, ukiamka utaona kumbe kila kitu hakipo kama kilivyo. Reality is an Illusion. Ukiwa kwenye ndoto, maisha ya ndoto yanaonekana ni kweli na haya maisha huyakumbuki wala huoni kuwa upo kitandani unaota bali unaona uhalisia mpaka ukiamka. Unaweza ukawa na hisia ukiwa kwenye ndoto, mfano mtu akikuchoma kisu unaweza kabisa kusikia maumivu lakini ni kwenye ndoto tu. Ukijikwaa unaweza kusikia maumivu lakini ni ndoto. Ukigusa vitu unahisi kabisa umevigusa japokuwa ni ndoto. Wengine wanaamka mapaka wanakuta na huu mwili wa maisha ya kawaida nao ulikuwa kwenye hisia na ukweli wa ndoto, mfano unakuta kwenye ndoto ulikuwa unaona unakimbizwa na unaamka unakuta unatoa kabisa jasho japokuwa ilikuwa ni ndoto. Mwili huu ni mtumwa wa Ufahamu na akili kwa ujumla, na hautambui tofauti ya ndoto na uhalisia.
Hivyo hata uhalisia au maisha ya kawaida tunayofikiri sio ndoto hatuna uhakika sio ndoto kwani wanadamu walioamka walitambua kuwa Maisha ni sawa na ndoto. Hakuna wakati ujao wala uliopita bali kuna wakati uliopo tu, wakati huu tu. Kutokana na series au mabadiliko ndio maana tunasema kuna wakati uliopita na wakati ujao lakini kama ulimwengu ungekuwa empty na leo ni kama jana na kesho ni kama leo tusingekuwa na muda.
Nadhani naenda mbali sana kuelezea lakini najitahidi mtu kuelewa kwani ni mengi sana wengi hawafahamu ila wanaishi tu kama walivyokuta jamii ambayo nayo haifahamu inavyoishi.
Umenijibu vyema.
Lakini ukiwa ndotoni pia unayaona maisha kama yalivyo sasa, ndio maana nikauliza. Twawezaje kujua hapa tupo ndotoni au la!
Kama ukiota leo hii tukiwa jf tunachangia hoja kama ilivyo sasa, tunaweza kuuliza maswali haya haya. Lakini itakuwa ndoto... Baadae ukiamka ndio utashtuka kumbe ulikuwa unaota.
Vipi kwa sasa Twawezaje kujua hii ni ndoto au la
Nipo hapa
Bado hujaweka neno lakini
Ngoja nikitulia nina dharura ya msiba
Pole sana kwa msiba mkuu. R I P kwa mwenzetu aliepumzika
Hakika ndugu yangu sasa upo kwenye hatua nzuri sana ya kuelekea panapotakiwa. madamu uanzapo kuhoji maswali hayo ni hakika upo katika hatua nzuri sana.
Kuna mambo mawili muhimu sana yanatakiwa kuyajua.
1. Ndoto itokanayo na hali ya kisaikolojia (Yaani akili inavuta matukio mbali mbali na kuyaunganisha katika series fulani). Hizi ndoto tunaweza kusema ni kulingana na taarifa zakidunia zilizoingizwa kwenye ubongo. Wakati mwingine ndoto hizi huhusisha movement ya mwili lakini si mara zote. Unapokuwa umelala akili huwa inafanya kazi kwa kiasi fulani japo kuwa mwili umetulia. Akili huwa ipo katika state inayoitwa dream state. Unaweza ukawa unawaza kitu fulani ukajikuta kinatokea kwenye ndoto au unaweza kuwa umebanwa mkojo na ukajikuta unakojoa. Na mambo mengine yafananayo na hayo.
2. Lakini kwa upande wa pili ni safari ya kiroho yaani nafsi inatoka katika mwili na kuvinjari sehemu tofauti tofatuti. Katika hali hii inakupa kujua na kufahamu kuwa maisha ya hapa duniani ni illusion tu siyo halisi. Katika ulimwengu huo wa kiroho hakuna time ni mazingira mazuri sana. Katika mazingira yale unaweza ukaona future ya ulimwengu wa mwili unaweza ukajua vitu vingi sana. Aina hii haihusishi movement ya mwili. Na ukikuta sasa upo aware utajua mambo mengi na kugundua dah!! kumbe dunia ndio iko hivyo!!?
Ngoja niishie hapa.
Nadhani ndugu ukisoma kwa makini hiyo post yangu imejibu kila kitu. Ndoto ya kiroho haihusishi movement za kimwili. Hayo ni mambo yaliyopo kwenye akili. Wakati mwingine watu walio na akili sensitive huwa wanaweza kuota movie walioitazama na wao kuvaa uhusika wake. ndoto yeyote inayohusisha movement za kimwili na kujikuta umechoa au kutoka jasho hizo zote zipo kwenye akili.Asante. Lakini vipi wakati mwingine ukaota labda unakimbizwa na mnyama mkali, na ukiamka unajikuta umechoka kweli hadi unatokwa jasho?
Nadhani ndugu ukisoma kwa makini hiyo post yangu imejibu kila kitu. Ndoto ya kiroho haihusishi movement za kimwili. Hayo ni mambo yaliyopo kwenye akili. Wakati mwingine watu walio na akili sensitive huwa wanaweza kuota movie walioitazama na wao kuvaa uhusika wake. ndoto yeyote inayohusisha movement za kimwili na kujikuta umechoa au kutoka jasho hizo zote zipo kwenye akili.