Nielewavyo mimi ni maneno mawili yenye maana zinazoelekeana lakini siyo sawa,mfano mtu anashuka shimoni,mtu anateremka bondeni; basi linapofika kituoni linateremsha abiria,ambapo polisi wa trafiki akisimamisha basi na kuna abiria waliozidi,basi huwashusha. Mkwea mti anaweza kushuka au kuteremka,anateremka pale anatumia ufundi wa kuteleza,la sivyo anashuka.