Tofauti ya neno "shusha" na teremsha

Tofauti ya neno "shusha" na teremsha

halati88

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
461
Reaction score
146
Wakuu haya maneno yana tofauti gani?na lipi ni sahihi kutumika?
 
Nielewavyo mimi ni maneno mawili yenye maana zinazoelekeana lakini siyo sawa,mfano mtu anashuka shimoni,mtu anateremka bondeni; basi linapofika kituoni linateremsha abiria,ambapo polisi wa trafiki akisimamisha basi na kuna abiria waliozidi,basi huwashusha. Mkwea mti anaweza kushuka au kuteremka,anateremka pale anatumia ufundi wa kuteleza,la sivyo anashuka.
 
Ili neno"SHUSHA"wanapenda sana kulitumia wanawake wakati wa tendo la ndoa.....!
 
Asante kidogo nimekuelewa,kwahiyo unataka kusema kwamba kushuka ni kitendo cha kuteremka kwa haraka au bila utaratibu maalumu?ama sivyo
Nielewavyo mimi ni maneno mawili yenye maana zinazoelekeana lakini siyo sawa,mfano mtu anashuka shimoni,mtu anateremka bondeni; basi linapofika kituoni linateremsha abiria,ambapo polisi wa trafiki akisimamisha basi na kuna abiria waliozidi,basi huwashusha. Mkwea mti anaweza kushuka au kuteremka,anateremka pale anatumia ufundi wa kuteleza,la sivyo anashuka.
 
shusha na teremsha ni visawe au sinonimu. hivyo visawe nimaneno yeye maana sawa. na katibu mkuu chawakama chuo kikuu Dar es salaam(UDSM)
 
Back
Top Bottom