Uchaguzi 2020 Tofauti ya sera za vitu na watu

zigii

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Posts
515
Reaction score
211
Nimefuatilia sana sera za hivi vyama viwili nimegundua kuna tofauti kubwa sana na hii inaweza kutuchanganya sisi wapiga kura tusijue sera ipi inatufaa kwa maslahi yetu. CCM wao wanasimamia maendeleo ya vitu CHADEMA wao wanasimamia maendeleo ya watu.

Hapa sasa bila wajuzi wa kuzichambua hizi sera wapiga kura wengi wenye kukosa maarifa ya utambuzi watashindwa kujua wapi panastahili kwenye maendelo ya mtu au vitu kwa wale wajuzi wa kuchambua sera tunaomba msaada wenu ili tupate mwangaza wa wapi tuelekee, nawakilisha.
 
Mkuu kasome Biblia au Quran utaona Mungu alianza kuumba vitu kabla ya watu. Ndio protokali zilivyo, weka miundombinu kwanza ili watu wapate pa kupita kujipatia maendeleo.

Yaani Mkuu anayekupa samaki hafai, upewe vitendea kazi ili uweze kuwafaidi samaki hata huyo mpaji akiwa hayupo.

Sasa Mkuu ukisahau yote niliyosema usisahau kwamba JPM anaangalia mbali sana, anaiona Tanzania ikijidhihirisha kama Eden Mkuu. JPM anatutaka tuione Tanzania iliyonona, yenye maziwa na asali. Ndio maana anathamini miundombinu ili kwa pamoja sasa tujijenge kwa urahisi na tuijenge nchi yetu iliyobarikiwa kumpata yeye kama kiongozi.

Anyway niwabakizie wadadavuzi wengine wamalizie, nisimalize uhondo wote wa hiki chuma kutoka Chato.
 
Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app

mkuu umepigilia msumari mmoja atakaebisha atakua alimsulubisha Yesu
 
hizo ni kauli mbili tofauti zenye maudhui moja, maendeleo ya vitu yanamlenga mtu direct na si wanya pia maendeleo ya watu yanalenga vitu ambavyo ndo msingi wa shughuli za kimaisha.

mtu tajiri utampima kwa vitu anavyomiliki, inshort hapa kuna watu wamekosa sera wakaamua kuchanganya maneno ili wananchi wasio na ufaham wadhani kuna jipya.
 
Mkuu kasome Biblia au Quran utaona Mungu alianza kuumba vitu kabla ya watu. Ndio protokali zilivyo, weka miundombinu kwanza ili watu wapate pa kupita kujipatia maendeleo.

Yaani Mkuu anayekupa samaki hafai, upewe vitendea kazi ili uweze kuwafaidi samaki hata huyo mpaji akiwa hayupo.

Sasa Mkuu ukisahau yote niliyosema usisahau kwamba JPM anaangalia mbali sana, anaiona Tanzania ikijidhihirisha kama Eden Mkuu. JPM anatutaka tuione Tanzania iliyonona, yenye maziwa na asali. Ndio maana anathamini miundombinu ili kwa pamoja sasa tujijenge kwa urahisi na tuijenge nchi yetu iliyobarikiwa kumpata yeye kama kiongozi.

Anyway niwabakizie wadadavuzi wengine wamalizie, nisimalize uhondo wote wa hiki chuma kutoka Chato.

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
Asante umeelezea vizuri sana sema tuu kuna watu hawapendi kusikia maneno kama hayo.
 
Kwa sera za ccm nilizosikia leo za tumeondoka corona tume dumisha amani sijui fyatua watoto manyonyo yapo ya kunyonyesha Lissu kabla ya misa ya kwanza kaisha mshinda mtu jamaa wamechoka sana wanaishi kwa mazoea eti jamani sera gani hizi?
 
Mkuu kasome Biblia au Quran utaona Mungu alianza kuumba vitu kabla ya watu. Ndio protokali zilivyo, weka miundombinu kwanza ili watu wapate pa kupita kujipatia maendeleo.

Yaani Mkuu anayekupa samaki hafai, upewe vitendea kazi ili uweze kuwafaidi samaki hata huyo mpaji akiwa hayupo.

Sasa Mkuu ukisahau yote niliyosema usisahau kwamba JPM anaangalia mbali sana, anaiona Tanzania ikijidhihirisha kama Eden Mkuu. JPM anatutaka tuione Tanzania iliyonona, yenye maziwa na asali. Ndio maana anathamini miundombinu ili kwa pamoja sasa tujijenge kwa urahisi na tuijenge nchi yetu iliyobarikiwa kumpata yeye kama kiongozi.

Anyway niwabakizie wadadavuzi wengine wamalizie, nisimalize uhondo wote wa hiki chuma kutoka Chato.

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
Sawa lakini uhalisia unahitaji msaada wa samaki kidogo na nyavu
 
Mkuu nimekusoma ukimuingiza mungu na bustani ya aden kwa binaadam haiwezekani
Mungu aliumba vitu kwanza kisha akamuumba binaadam aje avitumie bila gharama maana yake ,mungu alimuwezesha binaadam kwanza ili amudu maisha vitu alivyoviumba
 
Mkuu kasome Biblia au Quran utaona Mungu alianza kuumba vitu kabla ya watu. Ndio protokali zilivyo, weka miundombinu kwanza ili watu wapate pa kupita kujipatia maendeleo.

Yaani Mkuu anayekupa samaki hafai, upewe vitendea kazi ili uweze kuwafaidi samaki hata huyo mpaji akiwa hayupo.

Sasa Mkuu ukisahau yote niliyosema usisahau kwamba JPM anaangalia mbali sana, anaiona Tanzania ikijidhihirisha kama Eden Mkuu. JPM anatutaka tuione Tanzania iliyonona, yenye maziwa na asali. Ndio maana anathamini miundombinu ili kwa pamoja sasa tujijenge kwa urahisi na tuijenge nchi yetu iliyobarikiwa kumpata yeye kama kiongozi.

Anyway niwabakizie wadadavuzi wengine wamalizie, nisimalize uhondo wote wa hiki chuma kutoka Chato.
Mkuu unapisema mungu aliumba vitu kwanza una maana ipi? Vitu vinaumbwa au vinatengenezwa? Hata hivyo huyo mungu aliumba vitu hivyo kwa gharama ya kutoka wapi? Kama ni kwa gharama yake kwa nini wewe utengeneze vitu kwa kutukamua kwa mlolongo wa kodi nyingi? Kama unataka kumuiga mungu ni vizuri sasa tumia gharama zako kwanza
ILI UPATE MAZIWA MENGI MLISHE NGOMBE ASHIBE KWANZA
 
Huwezi kupiga ten percent bila kuanzisha miradi,tatizo miradi mingi ni ya upigaji,imejaa usiri na haukufuata utaratibu,miradi iende sambamba na maendeleo ya watu,kuna mtu jana katoa mfano wa ethiopia,fuatilia huo uzi.yafaa nini kulala kwenye ghorofa na ndani huna chakula
 
Mkuu unapisema mungu aliumba vitu kwanza una maana ipi? Vitu vinaumbwa au vinatengenezwa? Hata hivyo huyo mungu aliumba vitu hivyo kwa gharama ya kutoka wapi? Kama ni kwa gharama yake kwa nini wewe utengeneze vitu kwa kutukamua kwa mlolongo wa kodi nyingi? Kama unataka kumuiga mungu ni vizuri sasa tumia gharama zako kwanza
ILI UPATE MAZIWA MENGI MLISHE NGOMBE ASHIBE KWANZA

Sio lazima uchangie, unaweza kuonyesha uwezo mdogo wa ufahamu kwa kuchangia. Kama usinge changia hakuna ambaye angejua uwezo wako.
 
Nimefuatilia sana sera za hivi vyama viwili nimegundua kuna tofauti kubwa sana na hii inaweza kutuchanganya sisi wapiga kura tusijue sera ipi inatufaa kwa maslahi yetu. CCM wao wanasimamia maendeleo ya vitu CHADEMA wao wanasimamia maendeleo ya watu.

Hapa sasa bila wajuzi wa kuzichambua hizi sera wapiga kura wengi wenye kukosa maarifa ya utambuzi watashindwa kujua wapi panastahili kwenye maendelo ya mtu au vitu kwa wale wajuzi wa kuchambua sera tunaomba msaada wenu ili tupate mwangaza wa wapi tuelekee, nawakilisha.
Nadhani muda umefika wa Watanzania kuacha kuchagua chama Bali Sera za chama zinazoweza kutupa afueni hata tukiwa masikini.Mambo ya chama gani si mhimu majira haya tena. Tusihofu kujaribu Sera mpya kama zitaimarisha utu wetu na Mali zetu.Kuna baadhi wanakejeli Sera za wagombea wengine lakini ukisikiliza vizuri unawashangaa hata hao wamobeza
 
Sio lazima uchangie, unaweza kuonyesha uwezo mdogo wa ufahamu kwa kuchangia. Kama usinge changia hakuna ambaye angejua uwezo wako.

Hata sisi tumejua uwezo wako wa kuchanganya uwezo wa mungu na uwezo wa binaadamu
 
mtu kuendelea anahitaji vitu kwanza
mfano unataka mwanao atajirike unampa kitu mfano nyumba ya kupangisha,daladala,bodadoda nk hivyo vinaitwa viwezeshi au miundombinu ya kumsaidia kutajirika

SASA unakuta mtu analima sana lakini mazao yake yanaharikbika kwa kukosa soko linalosababishwa na ukosefu wa miundo mbinu kama barabara na madaraja ili aendelee na apate pesa unamjengea daraja na barabara mengine unamwachia mwenyewe

Bakheresa ni tajiri sababu ana vitu ana viwanda ana magari ana meli sasa mtu akisema maendeleo sio vitu kichwa chake kinatakiwa kubomolewa kiwekwe ubongo mwingine

Watu ni maskini kwa sababu hawana vitu

Wachaga wana msemo kuwa kama wewe unba akili kweli onyesha vitu ulivyonavyo kama magari,nyumba nk sababu kwao huamini kuwa akili ni kitu kinachoonekana sio cha kufikirika kilichojaa kwenye ubongo au cha mtiririko wa maneno matupu.Onyesha vitu ambavyo hiyo akili yako imezalisha vitu halisia vinavyoonekana

Kwa muktadha huo ukiniuliza Chadema wana akili au hawana jibu langu hawana akili sababu hawana vitu ikiwemo Jengo la makao makuu ya chama hawana wanapanga kijumba cha mkaa
 
Back
Top Bottom