Tofauti ya Simba SC na Yanga SC, Makocha pamoja na Mashabiki wao katika kupokea matokeo Uwanjani

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Hii ndo tofauti kwa Makocha pamoja na mashabiki wa Simba SC na Yanga SC katika kupokea matokeo uwanjani.

••Simba SC ikifungwa mashabiki wa Simba, wanaona ni hali ya mchezo wanakubali na kwamba mchezo wa mpira una matokeo matatu hivyo wanasonga mbele kwenye mapambano huku wakijipa moyo kuwa mechi ijayo watafanya vizuri kuweza kushinda.

••Yanga SC ikifungwa mashabiki wao wanaanza kuijia juu TFF kuwa inawahujumu na wala hawana muda wa kuwapa moyo wachezaji wao.

••Simba SC ikifungwa, Kocha Patrick Aussems anatoa sababu za kiufundi kwanini wamepoteza mchezo huo na kuahidi kufanyia kazi makosa.

••Yanga SC ikifungwa Kocha wao Mwinyi Zahera anaijia juu TFF, Simba na Waamuzi kuwa wanamhujumu asiwe bingwa wa TPL na hana muda wa kueleza matatizo ya timu yake kiujumla.

••Simba SC hata ifungwe, mashabiki wao wanaenda uwanjani kuipa support klabu, kwa maana wanajua Soka linataka nini na wanajua mpira pia.

••Yanga SC ikifungwa hawaendi uwanjani wanajazana kwenye vijiwe vya Kahawa huku wakisema TFF wale ni Simba na kudanganyana kila siku.

••Simba SC ikishinda wanasema Kahonga, mara TFF, mara magoli ya Penati na kulia lia kila wakati yaani full Malalamiko.

••Yanga SC ikishinda wanafurahi mno huku wakisema hakuna kama Yanga ilhali walipewa ubingwa mara tatu lakini hata Robo Fainali Hawakufika.

Mashabiki wengi wa Yanga hawana uelewa na masuala ya mpira ni vile wapo tu na wao waonekane..Lipi ambalo litainusuru hii klabu ya Yanga na Kocha wao kwa sasa..!
 
"Simba ikishinda Yanga wanasema simba kanunua, Yanga wanasahau na wao walifungwa taifa goli moja na Simba lakini hawasemi Simba iliwalipa kiasi gani cha fedha "
 
Mi mashabiki wa yanga sijawahi patana nao.wanamihemko afu kila kitu wanajifanya wanajua bila kuwa na hoja za kutetea.sio wote lakini watakuja kina prince nkuta apa utawaona hoja zao.yaani wanataka ushindi bila hoja nzito sisi mikia tunatulia mambo yanaenda
 
"Simba ikishinda Yanga wanasema simba kanunua, Yanga wanasahau na wao walifungwa taifa goli moja na Simba lakini hawasemi Simba iliwalipa kiasi gani cha fedha "
😱 😱 😱
 
Kwa maana hiyo Yanga wakifungwa basi jua wameuza mechi kama walivyo wauzia Simba.

Na wakishinda basi wamununua mechi..!
"Simba ikishinda Yanga wanasema simba kanunua, Yanga wanasahau na wao walifungwa taifa goli moja na Simba lakini hawasemi Simba iliwalipa kiasi gani cha fedha "
 
Simba wakifungwa hutaka kwenda hadi FIFA kudai points za mezani.
Simba misimu minne iliyopita ikifungwa ililalamika TFF na Bodi ya Ligi na Manara kitishia kutopeleka timu uwanjani hadi viporo vinne vya Yanga vichezwe.

Simba hii hii ikipeleka ombi la mda wa mchezo saa nane badala ya saa kumi linashughulikiwa lakini timu nyingine (sio Yanga) zilicheza saa nane ikiwemo Kagera wenyewe bila athari kutokea kiafya kusababishwa na pitch ya modern carpet.

Simba mashabiki wengi wana mdomo kama Man U, hivyo hujiona wao wana haki kuliko, huku Manara hata aongee ujinga lazima wajae.
 
AC Milan na Inter Milan wanatumia uwanja mmoja, San Sirio na kama Inter wakiwa wenyeji wanatumia jina la Giuseppe Meazza.

Na Liverpool na Everton waliwahi kutumia uwanja mmoja hapo mwanzo kwahivyo kutumia uwanja wa Taifa Simba na Yanga si jambo la kushangaza sana..!

La muhimu kwa sasa ni lazima Vilabu hivi viwe na viwanja vya mazoezi kwanza huku wakijipanga kuwa viwanja kwa ajili michuano TPL na Kimataifa.
Simba na Yanga wote wanatia aibu, timu zina miaka zaidi ya 80 HAZINA UWANJA, eti uwanja wa TAIFA wanapokezana kila msimu kuwa uwanja wa nyumbani hizi timu HOVYO KABISA
 
Simba na Yanga wote wanatia aibu, timu zina miaka zaidi ya 80 HAZINA UWANJA, eti uwanja wa TAIFA wanapokezana kila msimu kuwa uwanja wa nyumbani hizi timu HOVYO KABISA
Hata Italy hivyo hivyo..Serikali ndio ya kulaumiwa.. Manji alitaka kujenga Jangwani city akanyimwa kibari cha ujenzi
 
Hata Italy hivyo hivyo..Serikali ndio ya kulaumiwa.. Manji alitaka kujenga Jangwani city akanyimwa kibari cha ujenzi
Hakuwa na Nia huyo Kanjibai, kama alizuiliwa Jangwani, mbona ardhi pana sana?

Kumbuka aliahidi kuifanya Yanga Klabu bora Afrika Jee..!na hilo nalo alizuiliwa...!

Kazi kwako mkuu..!
 
Hakuwa na Nia huyo Kanjibai, kama alizuiliwa Jangwani, mbona ardhi pana sana?

Kumbuka aliahidi kuifanya Yanga Klabu bora Afrika Jee..!na hilo nalo alizuiliwa...!

Kazi kwako mkuu..!
Unakumbuka alitaka kufanya vipi? Alitaka kununua nyumba 50 zilizoko karibu na Yanga kwa 52B..alafu akachukue mkopo ajenge stadium pembeni maduka sio kule bondeni.. Alitaka kuikodisha Yanga kwa miaka kumi mtu masikini kama Akilimali anapata wapi nguvu ya kuzuia kama sio serikali. . Leo Yanga inatangatanga kajificha upuuzi mtupu
 
Wale Washabiki waliorusha makopo baada ya kichapo cha bao moja bila dhidi ya Mbao walikuwa wa Yanga?!
 
-Mashabiki wa simba wakifungwa wanang'oa viti
-Simba ikifungwa waandika barua FIFA kudai point za mezani
-Yanga wakiwa na vipolo vya mechi, simba wanagomea mechi zao kucheza mpaka vipolo vya ysnga viishe.
-Mashabiki wa simb as timu yao ikifungwa mara mbili mfululizo wanaana kulalamikia kocha afukuzwe.
-Mashabiki wa simba wanafurahia sana timu yao inapobebwa uwanjani mfano kupewa penalty ambazo sio halali
-Simba wapo tayari watoe mtu kafara(waue) ili timu yao ishinde
 
Mimi ni yanga damu lakini hakuna kocha zwazwa kama wa yanga.. Nannajua club inamvumila kwasababu ya ukata tu..!!
 
Simba na Yanga wote wanatia aibu, timu zina miaka zaidi ya 80 HAZINA UWANJA, eti uwanja wa TAIFA wanapokezana kila msimu kuwa uwanja wa nyumbani hizi timu HOVYO KABISA
Intermilan na ac milan hawana viwanja je! Hao ni bora kuliko simba na yanga!? Kombe lenyewe bingwa anapewa 80m ata kiwanja hakitoshi bado ramani [emoji3]
 
Mimi ni yanga damu lakini hakuna kocha zwazwa kama wa yanga.. Nannajua club inamvumila kwasababu ya ukata tu..!!
Dah, aisee umenena ukweli, amekuwa mkubwa kuliko Yanga
 
Wale Washabiki waliorusha makopo baada ya kichapo cha bao moja bila dhidi ya Mbao walikuwa wa Yanga?!
Tena makopo ya mkojo walimtupia manara na kocha wakadai aondoke nashangaa hawa mbumbumbu hawajioni
 
Zilipendwa hizo..kwa sasa tunazungumzia Kagera vs Simba SC na Mtibwa FC vs Yanga
Tena makopo ya mkojo walimtupia manara na kocha wakadai aondoke nashangaa hawa mbumbumbu hawajioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…