Tofauti ya Suzuki Escudo na Suzuki Grand Vitara/Vitara

Tofauti ya Suzuki Escudo na Suzuki Grand Vitara/Vitara

Hivi HALLY HENSEN ni nani kwenye suzuki?

HELLY HENSEN hausiki chochote na suzuki

hyo HELLY HENSEN ni kampuni ya norway inahusika na textiles na utengenezaji wa viatu vya michezo (wanamichezo)

ukiona suzuki imeandikwa helly hensen ujue imetumia bidhaa kutoka kampuni ya helly hensen katika ukamilishaji wake

na mara zote ikipigwa brand ya helly hensen bei yake inakuwa tofauti na nyingine sababu ile kwenye finishin kuna product maalumu toka helly hensen zimetumika

mostly siti za gari... vifuniko vya gear handle..na cover za steering wheel pamoja na roof liner
 
mkuu habari.... niende kwenye mada moja kwa moja

suzuki escudo , suzuki vitara, suzuki grand vitara hiyo ni gari moja hayo majina yasikuchanganye

first generation ilitoka 1988 ikiitwa suzuki escudo kwa soko la japan Japanese domestic market (JDM) na baadhi ya masoko machache kama asia spec na south america spec

ila kwa soko la US na EUROPE hii gari ilienda kwa jina la suzuki vitara

ilipofika second generation na kuendelea (now wapo forth) jina la suzuki grand vitara likazaliwa

ila ikabaki vilevile kwa soko la japan ikaendelea kuitwa suzuki escudo ila kwa US spec na UK spec ikaitwa suzuki grand vitara

kwahyo mkuu usihofu ukiona inaitwa escudo basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la japan (JDM) then ukiona inaitwa grand vitara basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la US na UK

ni kama tu toyota corola X assista ukiinunua ya asia spec itaitwa toyota altis

na ndio maana unaona hata kuna vitu ndani pamoja na uimara zinaweza tofauti kwa sababu kila moja hapo ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya soko fulani kutokana na vigezo husika pamoja na mazingira

ushauri ukitaka kuchukua ifate inayoitwa escudo sababu hii ni japanese domestic market (JDM) na mazingira yetu tanzania gari zinazoweza kuhimili shida zetu ni hizo JDM

Nina imani maelezo yangu yatakuwa yamekusaidia kidogo
Mkuu hilo ndio jibu. Hiyo ni gari moja, ila majina tofauti kulingana na masoko. Kuna wakati unakuta makampuni yanashirikiana kutengeneza gari, hivyo wanatofautisha majina kwa kila manufacturer lakini ni basically gari moja. Ila kwa Suzuki Vitara, hilo ni gari moja, kama ulivyoelezea. Ni tofauti ya majina tu kulingana na masoko.
Toyota IST in Japan, US ni Scion xA, Urope ni Urban Cruiser, Middle East ni Toyota xA. Ila ni gari lile lile tu
 
Mkuu hilo ndio jibu. Hiyo ni gari moja, ila majina tofauti kulingana na masoko. Kuna wakati unakuta makampuni yanashirikiana kutengeneza gari, hivyo wanatofautisha majina kwa kila manufacturer lakini ni basically gari moja. Ila kwa Suzuki Vitara, hilo ni gari moja, kama ulivyoelezea. Ni tofauti ya majina tu kulingana na masoko.
Toyota IST in Japan, US ni Scion xA, Urope ni Urban Cruiser, Middle East ni Toyota xA. Ila ni gari lile lile tu
yah mkuu .. pamoja sana nahisi hata kwenye vits ukichukua cha US spec hivi ndio huwa inakuwa yaris eeeh?
 
Mnyamaaa

BH791905_3f40a3.jpg
 
Mi namiliki Escudo vitara tangu 2006 nimeipaki inafanya shughuri za nyumbani siitembelei ila iko imara sana na siwezi kumuuzia mtu.kuna rafiki yangu alinunua grand kama miaka mitano baadae, alikuwa akinipigia simu niende kumvuta. kwenye efficiency especially kama we una shughuri mbalimbali na za masafa ya kwendea nyumbani mfano kama unaishi Dar unatumia kwendea kijijini na mizigo unabebea kinoma, N.B jitahidi kufanya service.
Escudo Vitara ndo gari gani? Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu
 
Ninayo Grand vitara. Nimeifunga na mkonga. Ni gari iko vizuri njiani. Hasa kwenye rough road imetulia sana. Engine ni kubwa na peformance ni nzuri njiani. Spare zake ni aghali kiasi unaweza ukabadili shockup za mbele na wish bone na mabush na raba zake kwa matumizi ya kawaida ndani ya mwaka mmoja na nusu. Ac yake ni deep freezer. Ina nafasi ya kutosha ndani kwa familia ya watu 5-6. Na mizigo yenu yote.
 
Kluger gari ya akina mama kwenda sokoni huwezi kuweka level moja Sawa na Escudo Massawe. Ile ni Land Cruiser ndogo. Kokote unakatiza bila wasiwasi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom