6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waungwana
Japo mimi sio mchambuzi mzuri wa mambo ya siasa, lakini nina imani kuwa wengi mtakubaliana na mimi kwamba utawala wa awamu ya nne na ya sita vinafanana sana, sema tofauti ipo kwenye jinsia ambapo awamu ya sita wanawake wameongezeka zaidi katika uongozi kuliko ilivyokuwa awamu ya nne. Hapo chini naorodhesha mambo ambayo yalifanyika awamu ya sita, yakatoweka awamu ya tano na kurudi tena awamu hii ya sita.
1. UZEMBE - Awamu ya nne kilikuwa na uzembe mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbali mbali, hadi kupelekea mingine kutelekezwa bila kumalizwa, au kuachwa kabisa kutekelezwa na wakati ilikuwa imeshasainiwa ianze kutekelezwa.
(1) Awamu hii pia ni hivyo hivyo uzembe umetamalaki, hakuna kinachofanywa kikamalizwa. wafanyakazi wa umma wanashinda wanapiga soga maofisini bila kufanyakazi zilizowapeleka katika ofisi hizo na kupelekea malalamiko kibao kwa watu wanaohitaji huduma zao kama vile uhamiaji, hospitalini nk.
Miradi ya BRT phase 3 ilianza kujengwa miaka 4 iliyopita mpaka leo watengenezaji hawajafikia hata 50%. Wao ni kuchimba chimba tu jiji zima bila kumaliza na kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hizo kwa njia ya gari na miguu.
Hapo sijazungumzia vumbi ambalo linasababisha magonjwa mbali mbali ya mafua na kikohoo. Halafu ujenzi wenyewe unaonekana ni wa sukuma twende. Namaanisha barabara hazina ubora kabisa.
2. UPIGAJI WA HELA ZA UMMA - Awamu ya nne hela za umma zilipigwa sana mpaka wengine wakajibebea hela hizo kwenye magunia bila kufanywa lolote na serikali.
(2) Na awamu hii pia hela za umma zinapigwa kweli kweli, kila mmoja anajitahidi kutumia mwanya wa ukimya wa serikali kupiga mamilioni ya hela za umma ili awahi kununua kiwanja huko Mbweni, ajenge na kuwa jirani wa raisi Samia.
3. KUONGEZA CHA JUU - Awamu ya nne wajanja wachache walitajirika kwa style ya kuongeza cha juu. Mfano unakuta ujenzi fulani ili ukamilike unahitaji Mil 100, basi wajanja watasema zinahitajika Mil 250 ili ile 150 ya juu iwe ya kwao.
(3) Pia awamu hii inaonekana swala la cha juu linaanza kuota mizizi mdogo mdogo na hakuna mfuatiliaji wa kukomesha tabia hiyo. Hata waziri mkuu akijitahidi kupambana na watu hao hujikuta anavyutwa shati na kushindwa kuendelea kufanya chochote kwa watu hao.
Anyway hizi awamu mbili zinafanana mambo mengi, lakini ili nisiwachoshe wasomaji basi acha niishie tu hapa.
Usiku mwema.