Ukiweza mpe vyote kwa kutanua wigo TIE kidogo viko ......ukichanganya mtoto anatanua wigo....hata vile vya Review ni vizuri pia.....Habari za asubuhi wanajukwaa,
Naomba kujua tofauti ya vitabu tajwa hapo juu maana naona kuna shule hasa hizi za English Medium zinatumia vitabu vya MEP kufundishia na zingine zinatumia vitabu vya TIE kufundishia
Kwa mfano mwanangu alikuwa anasoma shule flani (ameshamaliza)na walikuwa wanaasisitiza tumnunulie mtoto vitabu vya MEP, sasa vile vitabu nilitarajia mdogo wake (anasoma shule tofauti na aliyosoma kaka yake) atakuja kuvitumia sitanunua tena vitabu vingine sasa hii shule wao wanasema wanatumia vitabu vya TIE kufundishia watoto.
Mi naona wananichanganya tu maana vitabu vyote hivi vimeruhusiwa kufundishia sasa sijui tofauti yake ni nini?
Kwanini wengine MEP na wengine TIE?
Asante, wanasema mtoto lazima awe na vitabu vya masomo yote mkuuMEP ni kampuni binafsi, TIE vinatolewa na serikali
Vitabu binafsi huwa vina maelezo mengi, lakini TIE vinafuata syllabus kama ilivyo, ni kama vinatoa muongozo fulani
Hakuna vitabu sahihi mkuu, kila kitabu kina ubora na mapungufu yake
Kwani lazima ununue vitabu?
Mbona wengine tumepiga english medium bila vitabu? unatishiwa tishiwa tu ila sio kesi
Mtoto hawezi fukuzwa shule kama hana vitabuAsante, wanasema mtoto lazima awe na vitabu vya masomo yote mkuu
Shule za private kwenye matangazo na form wanasema shule Ina vitabu vya kutosha,mtoto akishaanza unakuta wanasema anunue vitabuAsante, wanasema mtoto lazima awe na vitabu vya masomo yote mkuu