TOFAUTI YA YA TAIFA STARS NA SENEGAL IKO HAPA

TOFAUTI YA YA TAIFA STARS NA SENEGAL IKO HAPA

hiram

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
266
Reaction score
393
Tarehe 23 June mwaka huu Taifa Stars itaumana na Senegal nchini Misri kwenye Michuano ya Afcon 2019 zifuatazo ni tofauti kati ya timu hizo

1. Wakati Tanzania wanajivunia kufikisha alama 18 kwenye Ranking za mashindano Caf ambapo mwakani wataingiza timu NNE, Wenzetu Senegal wanajivunia kuwa wa kwanza AFRICA kwenye RANKING za FIFA yaani washaachana na ushamba wa kupeleka timu nne hawana point hata moja kwenye 5-year caf Ranking hivyo wataendelea kuingiza klabu moja moja kwenye mashindano ya Caf kwa kuwa vijana wao wanatafuta kuonekana Ulaya wakati sisi tuna ddream za kuchezea Mazembe

2. Stars inafuzu kwa mara ya pili tangu 1980 na sasa 2018 wakati Senegal imeshiriki mara 14 ikitinga robo fainali mara tano na nusu fainali mara nne na fainali mara moja

3. wa tanzania wanaocheza nje ya nchi ni

https://us.soccerway.com/players/players_abroad/tanzania/

wasenegali ni kama wooote
https://us.soccerway.com/players/players_abroad/senegal/
kwa leo naishia hapo
 
Lazima timu ipate maandalizi bora na ya kutosha! Vi kamati vya ushindi vya kina Bashite havitasaidia kitu! Tukijipanga vema tunaweza tukafanya vizuri kiasi! Kila la kheri Taifa langu!
 
... nisingependa Tanzania kuanza na Senegal ama Algeria, watatupiga nyingi mno.
... Hii timu imevuka kibahati bahati, sasa huwezi kutumia bahati kila siku.
... Tanzania tujikite katika soka la watoto ili kuleta matokeo chanya kwa vilabu ambavyo vinatoa timu bora za taifa.
 
Sawa mkuu! Tofauti nyingine muhimu ni timu moja inatoka mashariki mwa Afrika na nyingine Magharibi.
 
Zambia walichukua AFCON 2012 wakiwa na Local players.. Wakiwafunga Ivory coast Drogba na Yaya ndani. . Acheni uoga.. Hilo Coulibary atawekewa oxygen kazi ya Msuva, Bocco, Farid na Captain Samatta
 
Back
Top Bottom