Tofuti kati ya Toyota Harrier na Lexus RX

RugambwaYT

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
1,397
Reaction score
1,899
Toyota Harrier, hasa 2nd generation, ni moja kati ya magari maarufu na pendwa saana hapa nchini na duniani kwa ujumla kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo muonekano wake, uimara wake, level of luxury na jinsi linavyokuwa comfortable wakati likiwa barabarani.

Hizi gari zinatengenezwa na kampuni ya Toyota kwa ajili ya masoko tofauti tofauti. Kwa soko la Ulaya na Marekani, gari hizi huitwa Lexus RX, na kwa soko la ndani la Japan, pamoja na baadhi ya nchi za Asia, gari hili hupewa jina la Toyota Harrier.

Hizi gari zimekuwa zikijulikana kwa majina mbalimbali kwa watumiaji wake, ambapo baadhi wamekuwa wakishindwa kuelewana kuhusu jina sahihi la gari hizi. Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa wapenzi wa gari hizi kuweza kupotezwa na kuuliziwa Harrier kwa jina la Lexus RX au Lexus RX kwa jina la Harrier. Kuna baadhi wanauziwa kwa jina la Lexus Harrier, au Harrier Lexus (kumbuka kuwa pamoja na kufanana saana kimuonekano, kuna tofuati kubwa kati ya hizi gari mbili ambazo zinaweza kubadilisha mawazo ya mnunuzi au mtumiaji).

Katika uzi huu, tutafahamishana jina sahihi kwa hizi gari, tofauti kubwa kati ya gari hizi kimuonekano na kwenye performance, mwisho, jinsi ya kutofautisha kati ya Lexus RX na Toyota Harrier hata kama label zimechanganywa. Karibuni saana tupeane ujuzi

Harrier

Lexus RX

Ingawa sina uzoefu wa haya magari ila lexus rx ni gari madhubuti na hata bei yake ipo juu kuliko harrier
 
Ingawa sina uzoefu wa haya magari ila lexus rx ni gari madhubuti na hata bei yake ipo juu kuliko harrier
Kabisa. Japo Harrier na Lexus RX ni basically gari moja, ila Lexus inakuwa na baadhi ya features za juu kidogo kuliko Harrier. So wauzaji wengi huwa wanabandua label za Harrier na kubandika za Lexus RX ili wauliuze gari kwa bei ya juu zaidi
 
Esp. kwenye siti cover lexus RX karibia zote unakuta ni leather huku ukija kwa harrier ni kitambaa
 
Leo ni kama ninaamka kutoka usingizini Mimi nikiona kama kitu kimoja tu
 
Nje ya tofauti ya Label kwa mbele na nyuma, kitu gani kingine waeza angalia hili kupata utofauti wa hizo gari mbili maana hata taa zake ni kama zimefanana ?
 
Esp. kwenye siti cover lexus RX karibia zote unakuta ni leather huku ukija kwa harrier ni kitambaa
Hii ni kweli kabisa. Lexus ni a luxury brand kwa US na Ulaya. Hivyo leather seats ni muhimu. Na hao jamaa wanapenda saana leather. Ni alama ya ufahari.
 
Leo ni kama ninaamka kutoka usingizini Mimi nikiona kama kitu kimoja tu
Ni kweli. Watu wengi ni kama wewe. Kibaya ni pale anapouziwa Harrier kwa bei kubwa kwa kuambiwa ni Lexus RX
 
Nje ya tofauti ya Label kwa mbele na nyuma, kitu gani kingine waeza angalia hili kupata utofauti wa hizo gari mbili maana hata taa zake ni kama zimefanana ?
Ukiangalia kwenye steering wheel kuna alama ya L, kwenye rims, kuna alama ya L, ukifungua mlango kumeandikwa Lexus, pia navigation screen, radio na button zote hapo mbele zinaandikwa kwa Kiingereza. Ukikuta Kijapani basi jua hiyo ni Harrier.
 
Safi mkuu, mada kama hizi zinatujenga usijeibiwa hapa mjini.
 
Sasa nmeelewa Kitu..juz kati mitaa flan Kariakoo....c nikaona Harrier imebandikwa Logo ya Lexus kwa nyuma na mbele..kumbe Mzee Mushi aliuziwa Harrier na sio Lexus kama ilivyo kwenye Logo....
Kabisa. Japo Harrier na Lexus RX ni basically gari moja, ila Lexus inakuwa na baadhi ya features za juu kidogo kuliko Harrier. So wauzaji wengi huwa wanabandua label za Harrier na kubandika za Lexus RX ili wauliuze gari kwa bei ya juu zaidi
 
Kabisa. Japo Harrier na Lexus RX ni basically gari moja, ila Lexus inakuwa na baadhi ya features za juu kidogo kuliko Harrier. So wauzaji wengi huwa wanabandua label za Harrier na kubandika za Lexus RX ili wauliuze gari kwa bei ya juu zaidi

Kwani kadi ya gari inakua imeandikwaje mkuu.?Toyota harrier au Lexus RX.

Point ya kuuliza hili swali nikujua kwanini wanunuzi wasisome kadi ilivyoandikwa?
 
hizi gari ni sawa kabisa jamani ni nembo tu..kuna harrier za 3gr 3.5
na kuna lexus za 2az...hata ulaya zipo lexus rx za 2az
inatakiwa mfahamu tu kwamba lexus ni toyota inayouzwa ulaya na america ya kaskazini..
zipo altezza za 2jz
na altezza lexus ya 3sge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…