RugambwaYT
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 1,397
- 1,899
Toyota Harrier, hasa 2nd generation, ni moja kati ya magari maarufu na pendwa saana hapa nchini na duniani kwa ujumla kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo muonekano wake, uimara wake, level of luxury na jinsi linavyokuwa comfortable wakati likiwa barabarani.
Hizi gari zinatengenezwa na kampuni ya Toyota kwa ajili ya masoko tofauti tofauti. Kwa soko la Ulaya na Marekani, gari hizi huitwa Lexus RX, na kwa soko la ndani la Japan, pamoja na baadhi ya nchi za Asia, gari hili hupewa jina la Toyota Harrier.
Hizi gari zimekuwa zikijulikana kwa majina mbalimbali kwa watumiaji wake, ambapo baadhi wamekuwa wakishindwa kuelewana kuhusu jina sahihi la gari hizi. Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa wapenzi wa gari hizi kuweza kupotezwa na kuuliziwa Harrier kwa jina la Lexus RX au Lexus RX kwa jina la Harrier. Kuna baadhi wanauziwa kwa jina la Lexus Harrier, au Harrier Lexus (kumbuka kuwa pamoja na kufanana saana kimuonekano, kuna tofuati kubwa kati ya hizi gari mbili ambazo zinaweza kubadilisha mawazo ya mnunuzi au mtumiaji).
Katika uzi huu, tutafahamishana jina sahihi kwa hizi gari, tofauti kubwa kati ya gari hizi kimuonekano na kwenye performance, mwisho, jinsi ya kutofautisha kati ya Lexus RX na Toyota Harrier hata kama label zimechanganywa. Karibuni saana tupeane ujuzi
Harrier
Lexus RX