Tofuti kati ya Toyota Harrier na Lexus RX

Tofuti kati ya Toyota Harrier na Lexus RX

Naweza kusema Lexus ni laxury version of Toyota.
Kabisa. Mwanzo zilikuwa ni model zile zile za Toyota ila zinawekewa some luxury features. Ila siku hizi kuna baadhi ya models wanatengeneza ambazo zinajitegemea, mfano hiyo RX. Sasa hivi haiko based kwenye models za Toyota.
 
Ukiangalia kwenye steering wheel kuna alama ya L, kwenye rims, kuna alama ya L, ukifungua mlango kumeandikwa Lexus, pia navigation screen, radio na button zote hapo mbele zinaandikwa kwa Kiingereza. Ukikuta Kijapani basi jua hiyo ni Harrier.
Na Lexus RX karibia zote zina CRUISE CONTROL wakati Toyota harrier hazina hicho kitu
 
Lakini nadhani ni hulka ya wabongo pia kupenda kuweka Hizo logos maana altezza kibao hapa mjini wameweka logo za Lexus is 200,wengine wana benz za kawaida ila wameweka logo ya AMG,kuna wenye bimmer za kawaida tu 3/5 series wanaweka logo ile Ya M3/M5 mpk nyingine bmw nilikuta imewekwa logo ya ALPINA.
Kwani hizo logo zinauzwa kariakoo?
 
Back
Top Bottom