Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye mito isiyopungua 100 isiyokauka kipindi chote cha mwaka. Lakini cha ajabu mji wa Morogoro, chini ya MORUWASA, unakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa maji. Kuna mitaa mingi sana, mathalani Bigwa, hukaa kwa muda wa miezi mpaka mitatu bila maji. MORUWASA, bila aibu, kila mwisho wa mwezi hupita na kusoma mita na kuwaletea bili za maji wenye mita .Miitaa kama Kihonda maji kwao ni almasi-hununua kwenye magari ya wauza maji, na uhaba huu wa maji yaelekea hauna jawabu. Ndoo MOJA ya maji, ya lita 20, huuzwa shilingi mia tano za kitanzania.
Huwezi kuwa nchi ya viwanda ikiwa maji yasiyohiyaji akili HAYAPATIKANI-just laying pipes na kusambaza kwa umma/watu!
Nionavyo mimi Shida kubwa kwa taasisi nyingi za umma, ikiwemo MORUWASA, ni: Kuwa na watumishi wengi wasio na uwezo,mizigo, wapiga dili na wanaofanya kazi kwa mazoea na pengine wenye maslahi na uhaba wa huduma za umma (mathalani wana magari ya kuuza maji, wana visima, au huduma ambazo zikiwemo kwenye idara za umma wanakosa dili). HAKUNA UBUNIFU, SOGA TU OFISINI NA kufanya kazi kwa mazoea-BUSINESS AS USUAL, ili mradi mwisho wa mwezi ufike waende kwenye ATM-kula kodi zetu.
Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paulo Makonda aliwahi kusema kuwa SERIKALI ina wafanyakazi wengi sana wasio na KAZI, MIZIGO. Nafikiri ni wakati muafaka kwa serikali kupitisha fagio la chuma, kubakisha watumishi wenye ueledi, tija na wabunifu, WENYE KUFANYA KAZI, SI KUPOKEA SALARI TU. Kuna mizigo mingi sana kwenye UTUMISHI wa umma. Magu pitia huku-watumishi waliopo, ambao si hewa, lakini hawana tija, mizigo, WAPOKEA SALARI TU BILA KUREJESHA HUDUMA ZENYE TIJA, WELEDI NA KWA WAKATI kwa jamii inayowalipa.
http://moruwasa.go.tz/home/index.php?option=com_content&task=view&id=47&Itemid=64