Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Ni Leo Asubuhi siku ya Jumatano siku ya tao ya mwisho wa mwaka 2016, yaani zimebakia siku 4 tu kumaliza mwa 2016 na kuanza mwaka mpya wa 2017.
Namuomba Mh. Rais JPM, aangazie macho yake kwa afya za wananchi, huduma za afya nchini hazirizishi hasa kwa maskini. Tumekuwa tukilalamika bila kuja na mbadala wa matatizo, lakini leo nakuja na mbadala. Watanzania wengi wenye ajira wanachangia BIMA ya AFYA kwa ajili ya jamii ya watanzania kwa ujumla. Ila kwakujua au kutojua fedha nyingi za Mfuko zimeelekezwa kwenye hospitali binafsi na mafamasi binafsi huku vituo vya serikali vikilia ukata, hakuna dawa vitendanishi wala vifaa vingine.

Mheshimiwa rais, fanya maamuzi fedha zote za BIMA ya Afya zielekezwe kwenye vituo na hospitali za umma utakuwa umesaidia wananchi na huduma zitakuwa bora zaidi kuliko sasa. Hospitali za umma zina wataalam wakutosha, ila huduma zinakwamishwa na kutokuwepo fedha za kutsha, mheshimiwa rais fedha BIMA zipo nyingi muulize Mama Makinda.
 
Mahakama ya mafisadi imeanzishwa na waziri wa sheria na katiba amesema bila kumun'gunya maneno mahakama imekosa kesi za kusikiliza kwa kuwa waliokuwa mafisadi wameogopa na kuacha kwa maana hiyo kulingana na kauli ya serikali kupitia waziri wa sheria na katiba Tanzania sasa hakuna mafisadi.nasema kweli mtupu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Sidhani kama hilio nalo ni jipu, kama watoto wapo na wazazi wanataka kuwasaidia watoto wao wapate mafunzo zaidi, hilo nalo ni kosa?
 
JIPU KUBWA JIPU KUBWA:
Naomba Mh. Makonda alitumbue mara moja..Halihitaji nguvu za Rais!!!
Hii ni kuhusu suala la kubandika matangazo katika kuta na kingo za madaraja katika jiji la Dar. Ukipita pale magomeni ama katika daraja la dart kimara na ubungo utachefuka. Watu wamebandika matangazo hovyo na yamegeuka uchafu na cha kushangaza hawakamatwi na wakati zipo namba za simu katika kila bango/tangazo. Hawa watu wanakosa ustaarabu hawalipi kodi za matangazo na Halmashauri zinakosa mapato.
Ningependa kukushauri mkuu...amuru kila halmashauri itengeneze mbao zake za matangzo tena za kisasa na watu waweke matangazo yao humo..sio kutwa kucha kutuchafulia mitaa yetu.
 
 
Kero kubwa ya nchi yetu ni ccm,ukiondoa ccm umeondoa uchafu wote Tanzania, Magufuli hawezi kuwa msaada kwa nchi yetu maana priority yake ni ccm na si Tanzania,watu wanatambulika kwa matendo yao siyo maneno
 
Tanzania bila; 1.Kufisadiwa 2.Kuibiwa 3.Kuchakachuliwa mali ya umma inawezekana.

Tanzania bila mambo ya kishenzishenzi na yasiyo mpendeza MUNGU inawezekana.
Hebu tuwaunge mkono wale viongozi wanao onyesha uthubutu wa kupambana na vitu hivyo
MUNGU tusaidie kututoa mapepo hayo ambayo yanasumbuwa watu wakidhani bila kufanya vitu hivyo maisha hayaendi.
Ninaomba na kuamini, Amen.
 
Ukishazaliwa ina maana Mungu amekamilisha uumbaji wake.

Mapepo tuliyonayo tumejitakia maana yanatokana na utawala unaotuongoza na kusikwa bila mapenzi ya Mungu
 
..ni kazi ngumu sana.

..kwasababu haki ya kukutana na kuchangiana/kubadilishana mawazo nayo inapigwa vita.
 
Kwanza Anza na huyoo ambaye unataka asaidiwe kuhusu kivuko cha mv daresalaam plus na nyumba za serikali and many more then hapo uzi wako utazidi kunoga kweli kweli... Sio ushabiki maandazi tuu hapa bana[emoji86] [emoji85] [emoji87] [emoji95]
 
Tanroads haiguswiii
 
Kama kwel maoni yanafika pahala usika, basi ishu ya bodi kukata 15% wanatumaliza wafanyakaz tulonufaika na mikopo hiyo. Ki ukwel kama wanatukomoa aisee
 

Mimi naona tumpe muda kidogo tupite kizungumkuti cha vyeti feki na madawa ya kulevya feki
 
Kwa muda wa wiki 2 sasa nimekuwa nikitembelea ofisi zenu katika moja ya mikoa ya kaskazini ili kununua return ticket ya Dsm, kwa kipindi cha kati ya tarehe 4/2 na 11/2.

Cha ajabu na kusikitisha mara kwa mara nimekuwa nikiambiwa labda uje kesho sababu makao makuu bado hawajaweka kwenye mtandao schedules za tarehe za mbele kuanza tarehe 9/2!

Na hata ukiingia kwenye website yao unashindwa kukata tiketi kwa tarehe hizo bila maelezo yeyote yanayoeleweka!

Wakati mashirika mengine ya ndege wala uhitaji kwenda ofisini, kuna options nyingi za kulipia tiketi.

Lawama hizi naitwisha menejimenti ya shirika, kama mmeshindwa kuwajibika si muachie ngazi!
============================================
ATCL kwa mapungufu haya hamtadumu
 
Wakazi wa Mbezi Wanapata Adha kubwa sana ya Usafiri hasa wakitaka kuja Mjini
Nauli imekuwa kubwa SANAAA!! tena SANAAA
Mbezi up to Kimara ni Tsh 400 ,then mabasi ya UDART ni Tsh 650 ,total ni Tsh 1050!!
Na zile daladala za kawaida zpo chache sna tena sana
Istoshe kwa ww ambaye unalipwa mshahara wa laki 3,4,5,6 Hyo n ndogo sana ila daaaah kwa ambao kpato chao ni kdogo km wanafunzi wa vyuo ,vijana ambao hawana kazi maalum ndyo Janga
Serikali mpo ?
 
Absolutely
 
Kero ni nyingi sana lakini kwa leo naomba nitoe kero moja tu ambayo ni Janga la njaa ambalo sehemu kubwa ya nchi mifugo inapata tabu sana, Watu ndo basi tena lakini bado tu baadhi ya wakuu wa mikoa wanasema hawana njaa ni ajabu kubwa na jambo la kushangaza sana viongozi kama hawa kiujumla hawatufai. Hii ndo kero kubwa sana kwangu.
 
Hilo ni jipu kubwa sana kwa kuwa wanaiba pesa za umma. Hawajatumbuliwa bado?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…