Toka lini Mwanaume anayejua kutafuta hela ukamtishia eti haumpi hela?

Toka lini Mwanaume anayejua kutafuta hela ukamtishia eti haumpi hela?

TOKA LINI MWANAUME ANAYEJUA KUTAFUTA HELA UKAMTISHIA ETI HAUMPI HELA!?

Leo 22:05hrs 19/11/2020

Ukimtishia Mwanaume anayejua kutafuta hela eti haumpi hela,hawezi kutishika,Chuma kinakusanya trillion 23 kwa Mwaka,sasa EU wanamtisha na 1.6 Trillioni? Kweli jamani!

Ni kweli trillion 1.6 inajenga fly over ya Ubungo, sasa Chuma kimetangaza kujenga fly over 5 kama ya Ubungo, Uhasibu, Fire, Mwenge na sijui wapi uko kuelekea mbagala.

Numbers don't lie, Mwaka 2019 Tanzania imepokea Watalii 1,527,000 na wameingiza 2.6 bilioni dolar, sasa 2.6 billioni zidisha mara rate ya leo 2312 kupata hela ya Kitanzania.

Ndugu zangu tusidhani wazungu wanaisaidia Africa hata siku moja, wanabeba rasilimali zetu kuliko kamsaada wanao dai wanatoa fanya tafiti zako ujiridhishe Thabo mbeki ripoti inasema Wazungu kila mwaka wamasomba Africa $700 millioni.

Ndugu zangu mkisikia tumepewa hela kiasi kadhaa na ulaya au America msifikirie yanakuja mabegi ya euro au dollar la hasha kinakuja ki dispatch tu kibarua tu,kinaenda kwenye Benki yao iliyopo hapa nchini,wanawaambia Tanzania ikitaka hela wapeni, Cha ajabu Tanzania ikitangaza kuuza hati fungani wananua wanadai wametupa pesa,

Ndugu zangu mkisikia nchi imesema imetupa mkopo sio hela zote za zile nchi bali kuna watu binafsi matajiri kwenye zile nchi wapo nyuma ya pazia wametoa,Sasa siku unaweza kuambiwa mwamkie yule unasema kwani nani yule,watakwambia yule ndio alikupa zile hela ulizoomba! Hapo ndio utajiuliza toka lini shetani akachukia dhambi!?

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
Ni kweli Kabisa. Mpaka saizi vitu vingi hawaelewi kama tumevibadilisha na tunajitegemea Mfano Uchaguzi Mkuu tumejitegemea 100%, NECTA 100%, TCU 100%, Ujenzi wa miundombinu 80% +15% kutoka china n.k.

Hata wenyewe wameelewa ukitaka kuishi kwa raha Duniani usiichokoze Tanzania utachukiwa Mpaka na Wananchi wako hukohuko kwenye mataifa yenu
 

Attachments

  • 9ebc6b4fd2ca4397b7998f5d4973259c.jpg
    9ebc6b4fd2ca4397b7998f5d4973259c.jpg
    43.1 KB · Views: 8
Kama tutawekewe vikwazo vya kiuchumi unatakiwa uje hao watalii hutawaona tena Tanzania
 
Kaka comment zote 34 hapo juu hakuna hata moja iliyounga mkono hoja yako. Hii nibkuonyesha hukufikiri vizuri kabla. WAHISANI wanapotusaidia/mabeberu wasipotusaidia ni watu muhimu sana japo tunawasema kwa lugha za dharau.
 
majuha kama wewe mnampoteza sana Magufuli. Tanzania hatuna sababu ya kuwa na aina ya uongozi unaovutana na nchi zilizoendelea kiuchumi. bado tunahitaji muda zaidi wa kushirikiana nao, tukijifunza kutoka kwao. ni kama mwanafunzi kuanzisha mvutano na mwalimu - utaishia kufukuzwa shule/chuo.

ficha UPUMBAVU wako.
Unataka ujifunze nini specifically
 
Haya sasa hii dunia ni kijiji.usije ukadhani utaficha kichwa kama mbuni halafu limwili lote liponje.Nani aliyewaambia muibe kura mnaingiza nchi nzima kwenye matatizo.Tamaa ndiyo hasara take eti nataka kuona kijani tu,ili iweje?
 
Kutegemew misaada ni ufukara mkubwa sana
unajitekenya na kucheka mwenyewe pole sana ndo huyo mumeo azidi kukutaftia hela za halali

Ila mshauri asitutoze kodi maradufu
 
"Ndugu zangu tusidhani wazungu wanaisaidia Africa hata siku moja, wanabeba rasilimali zetu kuliko kamsaada wanao dai wanatoa fanya tafiti zako ujiridhishe Thabo mbeki ripoti inasema Wazungu kila mwaka wamasomba Africa $700 millioni.

Ndugu zangu mkisikia tumepewa hela kiasi kadhaa na ulaya au America msifikirie yanakuja mabegi ya euro au dollar la hasha kinakuja ki dispatch tu kibarua tu,kinaenda kwenye Benki yao iliyopo hapa nchini,wanawaambia Tanzania ikitaka hela wapeni, Cha ajabu Tanzania ikitangaza kuuza hati fungani wananua wanadai wametupa pesa,

Ndugu zangu mkisikia nchi imesema imetupa mkopo sio hela zote za zile nchi bali kuna watu binafsi matajiri kwenye zile nchi wapo nyuma ya pazia wametoa,Sasa siku unaweza kuambiwa mwamkie yule unasema kwani nani yule,watakwambia yule ndio alikupa zile hela ulizoomba! Hapo ndio utajiuliza toka lini shetani akachukia dhambi!?"

UKWELI ULIOJIFICHA NA KUWASAHAULISHA WAAFRIKA KWAMBA KAMA WALITUITA NYANI, UPENDO KIASI CHA KUTUPATIA MISAADA UNATOKA WAPI? WALITUKATA VIUNGO VYA MWILI NA BADO WAATHIRIKA WENGINE WAKO HAI, LEO WANATUSAIDIA ILI IWEJE? NATAMANI WAAFRIKA WOTE TUNGEJITAMBUA NA KUWAAMBIA UKWELI WAZUNGU.
 
Uwezo wa kufikiria mdogo Sana.... Taifa lina uwezo wa kununua nje Miezi 6 tu... Wakipunguza hizo Euro ndio somo litaanza kuingia...... Usijisifu na PESA za madafu hazina issue mnaweza print mtakavyo kama Mzee Mugabe...
 
Umeongea kishabiki sana katika ulimwengu wa kileo kuwa na mahusiano mazuri ya diplomasia na nchi nyingine ni Faida sana, Hakika jeuri haijawahi kuleta hata mboga mezani Usiniambie kuwa umeona inshu ya msaada tu as impact hata hao wana ku motivate behind wanatumia izo kauli kisiasa ila wanajua fika impact za mabeberu. Usiwe mjinga wa kubeba kila unalosikia
 
700 million usd pesa ndogo sana wanayo somba ila vikwazo kwa nchi yoyote Africa inayotaka kutoka hata kwa inch ya kidole vikwazo lazima viwepo

wa Africa tunatakiwa kwanza tuondoe kizazi hichi cha brain washed natamani watoto wanaozaliwa 2020 waambie ukweli juu ya Africa kuanzia mashuleni hadi kwenye jamii

leo mtoto anafundishwa agricultural in japan 2002 itamsaidia nini na ndio matunda tunayaona yaani tunashindwa maamuzi mpaka mzungu aje ni ujinga

Demokrasia na mfumo wa vyama vingi ni pigo kwa Africa ni mbinu ya kuleta machafuko Africa nadhani tukikaa kama Africa na kuweka mipango yetu na kutazama haya mambo tutagundua haya leo angalia marekani kinacho endelea ingekuwa Africa mtu ameshakaa barabarani sasa watu wanajua labda ndio mfumo wa demokrasia kule kumbe mfumo wa siasa ni mmoja kwa dunia nzima sema tuu unatambulishwa kwa namna tofauti

leo angalia Nigeria wameingia kwenye mtego mdogo na wakajaa nadhani kuna nchi walidhani Tanzania itakuwa hivyo wakati na baadacya uchaguzi tunaomba Africa tuwe na umoja pamoja na upendo sisi adui yetu wote ni mmoja ambae anatufanya sisi wote tuwe maadui ili atawale vizuri

mtu alietesa babu zako tokea utawala wa mtu mweusi unaangushwa miaka kama 1200 iliyopita unadhani leo atakupa kitu kizuri na bora kuliko yeye?

kufika kwa wazungu Africa sidhani kama ilikuwa ni kufanya biashara ya utumwa ila walitaka kuanzisha makazi kwa kuwatoa watu weusi kwenye ardhi yao ndio kitu kigumu walichobuma angalia zimbwabwe,south africa na hata nchi nyingine kama Botswana sasa leo unaniambia kwamba anaalemgo mazuri na sisi issue ya population control ni agenda ya kusaidia mpango wa uzazi wa Africa kweli?

Na kutuacha bado kwenye himaya zao ndio hii mifumo tunayo ona ikaanzishwa kwa haraka nadhani wazungu waliofikiria hivi walikuwa wana akili sana kutubana kwenye elimu,siasa na uchumi ukizidisha dini ndio hoii kabisa kuna kiongozi wa Africa alisema adui mkubwa wa maendeleo ni Ujinga,maradhi na umaskini Africa haikuwa masikini kama hivi leo Africahaikuwa na magonjwa kama leo kama kweli utakaa na kufikiria sidhani kama bado utakuwa unataka control yao kila nikiona taarifa ya habari kuhusu Africa ughaibuni ni ugomvi,mapigano na umaskini natamani waafrica tufunguke

mtu alisema natamani wazungu watutawale tena mimi naona natamani tupewe taarifa za kweli kuhusu Africa kwa mara nyingine Africa tupewe elimu yetu iliyofungiwa kwenye nchi zao tupewe historia yetu tuambiwe namna gani Africa ilitawala dunia namna gani wazungu walifundishwa ustaarabu na waafrica namna gani chuo cha kwamza duniani kiliwafundishwa watu wote duniani na namna gani africa ilikuwa mfalme wa matibabu na madawa

hebu tufungueni akili Africa hakuna atakae kuja kutuokoa hapa leo mbona marekani isiingie mahakama ya kimataifa kama raisi wao ana force hivyo ila ingekuwa Africa ni shidaa wengine wange pelekana huko ni tatizo hilo

Africa tuwe na mfumo mzuri wa siasa zetu ikiwezekana uchumi na hata kitaaluma haiwezekani mpaka leo unasoma kuhusu dutch impact kwa south Africa for what and for who na ina saidia nini tukianza kuwapa ukweli watoto wa 2020 yaani watoto wote chini ya miaka 5 ikifika mwaka 2040 hadi 2060 tuna kizazi ambacho kinajua ukweli juu ya Africa

leo msomi ndio bullet proof ya mfumo wa mzungu inasikitisha sanaa
 
Tunazo rasilimali nyingi za kutosha kuweza kuiendesha nchi hii, tunao uwezo wa kujitegemea na hata kuwasaidia hao mnaowaabudu huko Ulaya.
 
majuha kama wewe mnampoteza sana Magufuli. Tanzania hatuna sababu ya kuwa na aina ya uongozi unaovutana na nchi zilizoendelea kiuchumi. bado tunahitaji muda zaidi wa kushirikiana nao, tukijifunza kutoka kwao. ni kama mwanafunzi kuanzisha mvutano na mwalimu - utaishia kufukuzwa shule/chuo.

ficha UPUMBAVU wako.
Wewe ndio mpumbavu!

Tz haihitaji kuingiliwa mambo yake ili kushirikiana na EU!

Ujinga huo wanao viongozi wa chadema tu
 
Umeongea kishabiki sana katika ulimwengu wa kileo kuwa na mahusiano mazuri ya diplomasia na nchi nyingine ni Faida sana, Hakika jeuri haijawahi kuleta hata mboga mezani Usiniambie kuwa umeona inshu ya msaada tu as impact hata hao wana ku motivate behind wanatumia izo kauli kisiasa ila wanajua fika impact za mabeberu. Usiwe mjinga wa kubeba kila unalosikia
Wewe ni hasara kwa taifa na ni moja ya watu wenye roho ya kimaskini sana
 
Chadema wanalilia misaada wapeleke wapi?

Nashindwa kuelewa kwa nini wameumia
Wewe ndio mpumbavu!

Tz haihitaji kuingiliwa mambo yake ili kushirikiana na EU!

Ujinga huo wanao viongozi wa chadema tu
 
Ilani itakuwa ngumu sana kutekelezeka kwa hata 60%!
Hiyo 60% hatujawahi kufika pamoja na msaada na mikopo yao, leo hatupew ndo tutafika?
Nasikia wabunge wanalalamika huko kwa kupewa mil50 badala ya 90 kwa ajil ya posho na gar
 
Mluguru taratibu, teuzi hakuna, ukiropokaropoka ka umekunywa gongo ya Mkundi, watakufukuza hadi uanachama ushindwe kumng'oa Abood!😀

Halafu huku huonekani, hakuna wajumbe!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom