Toka Mitandaoni, waTanzania tunataka nini toka viongozi wa upinzani?

Toka Mitandaoni, waTanzania tunataka nini toka viongozi wa upinzani?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Salam za pasaka na mwezi mtukufu.

Nianze kwa kuwauliza hivi nini tunachokitaka toka kwa wanasiasa wa upinzani? Nikapita mitandaoni nikaangalia page kadhaa then nikapita na page za wanasiasa nikagundua kuwa wananchi hatuna tukitakacho na tupo kulaumu.

Usichukie ilikuwa hivi.
Nilipita page ya Zitto kabwe, nikakuta amepost uchambuzi wa ripot ya CAG na Ile hotuba ya PM juu ya mwelekeo wa bajeti ila response ilikuwa negative. Mara Zitto kabwe amenunuliwa mara Zitto Kabwe hataki kudai Katiba Mpya.

Nikapita na kwa Lema kidogo, nikakuta mabango yale Yale, sijui unaongea ukiwa mbali, Rudi kwanza, Mara crdb wanakudai, hoja zake hazijibiwi Wala kujadiliwa.

Nikapita na Martin Maranya, nikakuta kapost maneno ya sugu kwamba "Kitila alinifuata na blank cheque niweke kiasi nikitakacho nihamie ccm". Majibu ya wabongo "Uongo". Hukufika tu Bei?

Nikapita na Mwananchi nikakuta wamepost habari ya Mbowe kupiga kuonewa kwake na kuwahakikishia wafuasi wake kuwa yeye sio gaidi. Majibu ya likuwa. Ni huruma tu ya mama kuwa nje.
Mara Mbowe ongelea ugumu wa maisha yetu achana na hayo.

Sasa nakuja kwenu.
Zitto Kabwe anapojadili bajeti na ripoti ya CAG yupo wrong ?
Lakini tunamtaka Mbowe atoe maoni yake juu ya hilo Jambo ambalo kwa ZZK ni baya?
Kuna tatizo mahala.

Hawa wapinzani tunataka wajadili nini?
 
Hata wenyewe hawajui.

Wanaandika hashtag ya katiba mpya, mtu wa kijijini akiisoma haoni connection yake na maisha anayoishi, lakini akimuona Waziri wa maji anakuja kuzindua mradi, anaelewa, maana ana shida na maji, akimuona Waziri wa elimu anamuonyesha madarasa ya kisasa ya Samia, anasema yes, akiona tarura wanapitisha greda, anapeleka mazao kwa barabara safi, anaelewa, anaona dispensary inajengwa anaelewa, anamuona bashe anapita na maafisa ugani anaelewa, Sasa umjazie buku jipya lililoandikwa katiba mpya la nini?

Akilisoma anaona ni Mbowe na genge lake wanataka madaraka, na Mbowe akiyapata, inabidi Kodi yake ikamlishe Mbowe na kumnunulia konyagi pale dodoma
 
Zzk anajaribu kuongelea hali ya maisha ya waTz lakini wanaoccoment kwake wanataka kumsikia akizungumzia katiba,kususia nk.

Mbowe anazungumzia katiba lakini wanaoccoment wanataka azungumzie hali ya maisha ya wananchi
 
Back
Top Bottom