Toka nakua na mpaka sasa sioni faida ya Mwenge wa Uhuru

Toka nakua na mpaka sasa sioni faida ya Mwenge wa Uhuru

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Kwa vyovyote vile nitakuwa wa mwisho na wakwanza kuajua faida za mwenge. Sioni faida wala umhimu wa huu mwenge kuwepo, mwenge umekuwa na karaha pale unapoenda sehemu yeyote.

Kuna siku nimeitwa na mkuu wa Wilaya, wilaya flani akisema nitoe mchango wa mwenge nikamwambia mwenge unabajeti yake inakuwaje wananchi wachangie kutoka kwenye mifuko yao ili hali mnajua halizetu siyo nzuri mnataka hata hiki kidogo tunachopata mkichukue tutaishije na familia zinahitaji mahitaji kila kukicha.

Mkurugenzi akasema yeye hajali hilo anachotaka ni mchango, akaniambia mwenge hauna bajeti unaghamiwa na wananchi wenyewe siyo serikali.

Nikamwambia Mkurugenzi kwa sababu unalazimisha niandikie barua ya kuniomba huo mchango na mimi niwe najua nachangia mwenge kwa msingi upi!

Huwezi amini alikataa kunipa barua na akasema kama sitaki nitaona tutakufuatilia kuhusu biashara zako.

Ndugu zangu haya ndio yanayoendelea kwenye maisha ya utafutaji dhidi ya watawala, sasa kama mimi ambae najihangaikia napigwa biti namna hii kuhusu kunichunguza kisa nimegoma kile anachodai kwa nguvu bila sababu za msingi na wala bila kuwa na ushawishi wowote kwanini nitoe hiyo pesa ya mwenge je, akikutana na mtu ambae anafanya biashara gizani na mkwepa kodi mfano wafanya biashara wakubwa hawa, unadhani nini kinawakuta hasa baada ya mwenge kuja kwenye maeneo yao mfano Wilayani n.k?

Huu mwenge ni upigaji tu wala si kumulika majizi kama Mwl Julius K. Nyerere alivyo tukalilisha kwenye utawala wake.

Sasa umegeuka kuwa fulsa kwa wale wa upande wapili na umekuwa ndio kichaka cha kuficha upuuzi wao.
 
Back
Top Bottom