Tanzania ina mahusiano mazuri na nchi nyingi za kiarabu. Mataifa mengi ya kiarabu yenye mlengo wa kushoto yamewahi kuisaidia sana Tanzania pale ilipokumbwa na changamoto za kifedha na kiusalama. Nadhani hili tuliweke wazi kabisa ili kuweka kumbukumbu sawa. Watanzania hawachukii waarabu, bali mbinu za kishenzi zinazotumika na baadhi ya mataifa ya kiarabu kuhatarisha uhuru wa nchi.
Wakati tunapambana na nduli Idd Amin, Tanzania ilikuwa haina fedha wala silaha za kutosha. Algeria ni moja ya taifa la kiarabu ambalo lilisimama kidete kuisaidia Tanzania kijeshi, kidiplomasia na kifedha. Ilifika kipindi baadhi ya magazeti ya kitanzania yaliandika propaganda kusema waarabu ndiyo wanamsaidia Idd Amin. Kitendo hiki kilimkera mno mwalimu Nyerere akawafuta kazi baadhi ya wahariri. Algeria walisimama na sisi hata pale ambapo mataifa mengine ya kiarabu na kiislamu yalipo muunga mkono Idd Amin katika uvamizi wa Tanzania.
Wakati mwingine ni ule ambapo marehemu Saddam Hussein wa Iraq alipotuma msaada wa mafuta mengi mno kwa Tanzania kipindi nchi imefilisika. Nchi ilikuwa imesimama na mahusiano mazuri ya kidiplomasia na wema wa watanzania vilichangia mno Tanzania kupewa msaada na mataifa mengi duniani, yakiwemo yale ya kiarabu.
Baada ya Mzee Nyerere kuvunja idara ya usalama wa taifa miaka ya 70's na kuwaondoa wakina Mzena, majasusi wengi wa Tanzania walipelekwa mafunzo nchini Lebanon. Wakati huo Lebanon ilikuwa ni nchi haswaa na haijaharibiwa vita pamoja makundi ya migambo wa kiislamu. Cohorts zilizopelekwa Lebanon, East Germany, Israel, Urusi, Czechoslovakia na Cuba ndiyo zilitoa watu bora kabisa waliosaidia Tanzania kwenye kupambana na vitisho mbalimbali vya usalama hapa nchini.
Nadhani kuhusu hili la bandari, tusipende kujumuisha mambo kwamba waarabu wote ni wabaya. Haya yanayofanywa na DP World yalianza kufanywa na mataifa kama Uingereza, Ufaransa na Marekani miaka zaidi ya miamoja iliyopita. Walitumia dini, fedha, vitisho na ulaghai katika kuyatawala mataifa ya duniani. Hichi ndicho UAE wanakifanya sasa. Wanatumia mwamvuli wa dini, rushwa, ulaghai na vitisho dhidi ya mataifa ya Afrika wakianzia kule Djibouti, Sudan, Somalia na sasa wamefika Tanzania.
Don't get it twisted. Watanzania wengi hata wale ambao wanafuata dini ya kiislamu hawaufahamu huu ukweli ambao ninakueleza sasa. Mataifa ya kiarabu hayafanani "Arab" ni jumuishi "Generic". Hivyo kuwaweka wote kwenye kundi moja utakuwa hutendi haki. Hata "Africa" ni neno jumuishi "Generic", linalomaanisha wakazi wa barani la Afrika ambao kiasili ni weusi. Ndani ya "Africa" kuna makundi "sub-groups" saba, ambayo ni Nilotes, bantus nk. Hata waarabu wenyewe wako kwenye makundi matatu ambayo hayafanani kabisa na yanavutana.
Kuna Arab Petraea, Arab Desserta na Arab Felix. Haya makundi ni tofauti na hayafanani japo huwa wanalazimisha. Waarabu wa UAE wako kwenye kundi la Arab Desserta, kiufupi hawapatani sana makundi mengine ya kiarabu. Sababu ni za kihistoria. Mpaka sasa haya makundi yanavutana, wakati mwingine yanafika mbali hadi kuchinjana kama kuku. Nafahamu wengi tumekerwa mno na DP World, ila ninacho kushauri hapa ni hiki tu, stop putting people in a monolith.
Tanzania kama nchi hatufungamani na upande wowote ule. Kama tutafungamana basi ni kwa maslahi mapana ya watanzania wote, siyo viongozi au kundi fulani. Hata UAE kushirikiana nao siyo kosa, tatizo ni tunashirianeje nao ? Siku za hivi karibuni nchi kama UAE, Saudi Arabia na Qatar zimekuwa na rekodi mbaya ya kuvuruga amani duniani na kusababisha maelfu ya vifo kupitia fedha zao za mafuta. Wamesababisha matatizo Middle-East na sasa wamefika Afrika. Tanzania tumeingia kichwakichwa tukizingatia fedha na maslahi bila kuzingatia usalama wa nchi kwa muda mrefu. Binafsi nadhani hili ni tatizo kubwa.
Ingekuwa ni kipindi cha Mzee Nyerere sidhani hata kama mawaziri wangediriki kwenda kwenye Dubai Expo, let alone kusimama kupiga picha na viongozi wa UAE. Hata huu mkataba sidhani kama wangediriki hata kumfuata kule Ikula na kumwambia wasaini, angewafukuza kama mbwa.
If we stand on founding principles of this nation, countries within Arab Desserta can never be our ideal development partners. Its even abominable that we have endowed them with unlimited access to strategic and critical gateways like ports.