Tokea Malinzi aondoshwe, Yanga wanaboronga

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Tokea aliyekuwa rais wa TFF Malinzi kuondoshwa madarakani timu za yanga na kagera wameanza ligi vibaya ni dhahiri yanga na kagera wanafanya vibaya kwenye ligi na ni jambo la kushangaza.

Imekuwa ikizoeleka kwa nyakati hizi yanga inashika nafasi ya kwanza huku kagera akiwa nafasi ya nne lkn imekuwa sivyo ndivyo klabu ya yanga inajikongoja na kagera wameshika mkia

Je yanga na kagera wana mmiss Malinzi ?

Yanga haijaboronga, inazidiwa pointi mbili tu na anayeongoza ligi.
Imecheza mechi tano, imeshinda mbili vs Njombe mji, Ndanda fc.
Imesuluhu mechi ngumu tatu vs Lipuli, Majimaji, Mtibwa.
Ina pointi tisa.
Ina magoli ya kufunga matatu
2 Ajib, 1 Ngoma.
Imefungwa magoli mawili.
Inatofauti ya goli moja. 3 - 2
Iko nafasi ya Sita katika msimamo wa ligi.
Ipo chini ya kocha mahili Lwandamila.
 
Kocha mahili ndy nani?
 
hali ni ngumu kwa yanga mwaka huu
 
Tofauti ya point mbili nyie wavaa jezi kwa maagizo ya waganga mnapiga kelele utafikiri mmechukua ndoo tayari.
Ligi ina mechi nyingi. Siku zote huwa mnaongoza lakini mwishowe pumba na mchele hujitenga
 
Tofauti ya point mbili nyie wavaa jezi kwa maagizo ya waganga mnapiga kelele utafikiri mmechukua ndoo tayari.
Ligi ina mechi nyingi. Siku zote huwa mnaongoza lakini mwishowe pumba na mchele hujitenga
Hata msimu huu, Yanga mnachukua ndoo ya ubingwa wa ligi.
Simba inawawekea nafasi yenu tu.
Lwandamila Oyee...!
 
Hata msimu huu, Yanga mnachukua ndoo ya ubingwa wa ligi.
Simba inawawekea nafasi yenu tu.
Lwandamila Oyee...!
Endeleeni kusikiliza nyimbo za Haji Manara.
Unatania lakini mwisho wa msimu Itakuwa hivyo. Ba Yanga akikosa ubingwa, utaenda Singida United au Azam
 
Endeleeni kusikiliza nyimbo za Haji Manara.
Unatania lakini mwisho wa msimu Itakuwa hivyo. Ba Yanga akikosa ubingwa, utaenda Singida United au Azam
Umesema ukweli, wanaotarajia kuchukua ubingwa wa VPL ni Yanga, Azamu na Singida United.
Wengine ni wasindikizaji tu.
 
Malinzi alikuwa anacheza namba ngapi kwenye timu?
 
Malinzi alikuwa anacheza namba ngapi kwenye timu?
Matopeni hawajiani hata kidogo. Jana wamegoma kutumia jezi ya away maana hizo nyekundu zililala kwa sangoma.
Wakatembeza hela kwa kamisaa na viongozi njaa wa Stand United ili liende hivyo hivyo licha ya jezi kufanana sana. Harafu wanataka muujiza wa Second Refaree kuona offside
 
Mwaka Jana kipindi kama hiki Yanga ilikuwa hoi bin taabani ikizidiwa na Simba zaidi ya pointi 8.

Kipindi hili Malinzi hayupo inazidiwa point 2
 
Sasa Simba mnataka Yanga iwe vizuri ichukue kombe Mara ya NNE mfululizo. Arrrghh
 
Tofauti ya point mbili nyie wavaa jezi kwa maagizo ya waganga mnapiga kelele utafikiri mmechukua ndoo tayari.
Ligi ina mechi nyingi. Siku zote huwa mnaongoza lakini mwishowe pumba na mchele hujitenga
Mbeleko imekatwa rasmi pambana na hali yenu chura churani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…