Tokea umejua kiswahili fasaha kimekusaidia nini?

Tokea umejua kiswahili fasaha kimekusaidia nini?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Mimi nilijua ukijua kuandika vizuri kiswahili kinalipa, sio kila mtu anaweza kuandika vizuri, hata huko Ulaya Kingereza sio wote wanaondika vizuri.

Sasa wewe mwenzangu unayekuja kutakebei kwa Kiswahili chako fasahaa kimekupa nini? Wenye lugha zao wanavozidi kuzipa teknolojia na maendeleo huku wakizidi kukupa misaada.

Kama lugha inakulisha basi utakuwa tajiri.
 
Eeeeeeeeeeeeeeeh

Jf uwanja wa mapambano,vichambo,masengenyo
 
Mimi nilijua ukijua kuandika vizuri kiswahili kina lipa.sio kila mtu anaweza kuandika vizuri,hata huko ulaya kingereza sio wote wanaondika vizuri.

sasa wewe mwenzangu unayekuja kutakebei kwa kiswahili chako fasahaa kimekupa nini !.

Wenye lugha zao wanavozidi kuzipa teknolojia na maendeleo huku wakizidi kukupa misaada.

kama lugha ina kulisha basi utakuwa tajiri
Ifikie sehemu ukiambiwa na kumaizi kwamba kitu hujui,ni vema ukakubaliana nacho tu.Nitakueleza kidogo iwapo utaonesha haujui kiswahili kizuri cha mawasiliano/fasaha
-ukiandika kiswahili kibaya/kisicho fasaha unaonekana mdumavu wa akili.Lugha uliyozaliwa na kujifunza kuongea na kuiandika,inakushindaje?Labda uwe umejifunza ukubwani au weye bado ni mtoto(totoo).
-Si mwepesi wa kutaka kujifunza usahihi wa unachokiongea au kuandika.Huo ni uzembe sana.Ni sawa na kujisaidia kwenye bukta uliyovaa.
-Unaonekana unarukia mambo usiyoyaweza au ambayo si kiwango chako.Lugha huiwezi,kwa nini usiandike na kuongea unachokimudu?
-Kukosolewa kwamba umekosea na kubisha kwa kukaza shingo na kuwa mkali nao ni ujinga.Hupendi kujifunza.Ni heri ujifungie chumbani uishi ulimwengu wako.
Kuna mengi ila kwa sasa ni hayo tu.
 
Kama uko poa utaenda nje kufundisha kiswahili. Ila tatizo letu ni lazima uwe na refa.
 
Mimi nilijua ukijua kuandika vizuri kiswahili kinalipa, sio kila mtu anaweza kuandika vizuri, hata huko Ulaya Kingereza sio wote wanaondika vizuri.

Sasa wewe mwenzangu unayekuja kutakebei kwa Kiswahili chako fasahaa kimekupa nini? Wenye lugha zao wanavozidi kuzipa teknolojia na maendeleo huku wakizidi kukupa misaada.

Kama lugha inakulisha basi utakuwa tajiri.
Tatizo mnapenda kuandika wakati lugha haipandi. Kama hujui lugha acha kuandika, uwe msomaji kama mimi. Ila ukiaamua kuandika na ukakosea lazima tukusahihishe.
 
Kujua lugha ya kiswahili kwa ufasaha inasaidia kuwa na wigo mpana kujiajiri au kuajiriwa. Kiswahili fasaha kinafanya ujiamini kuandika na kuongea mbele za watu wengi. Mfano hawa maafisga habari wa timu au idara fulani kama si kujua kiswahili fasaha nani anaweza kuwasikiliza wanachoongea mbele ya vyombo vya habari? Huko nyuma enzi za mwalimu na mwinyi ilikuwa hupati kazi kwenye media za serikali na chama kama hujui kuandika na kusoma kiswahili kwa ufasaha.
 
Andika kiswahili kibovu utakavyo ila usituwekee x kwenye s...plzz
 
Duuuh kiswahili fasaha umekua kamusi
Kujua kiswahili fasaha km kle cha kwenye kamusi ya Tuki

Wangekua wanajua kiswahili fasaha saiv wangekua China, Marekani na uraya wanafundisha kiswahili km wenzao wakenya ambavyo wamejazana uko mashuleni na vyuoni wanafundisha
 
Kumezuka mtindo wa kihuni kuandika meseji kwenye simu kwa kufupisha maneno, tena maneno mengine ni magumu kusomeka kama mtu hajui hayo maandishi ya kihuni. Unamuandikia mama au baba ujumbe mfupi kwenye simu kwa kutumia huo mtindo, hao wazazi wataelewa nini ? Huo ni uvivu wa kuandika na uharibifu wa lugha fasaha ya kiswahili
 
Back
Top Bottom