Tony Atlas kutoka kuwa mcheza mieleka maarufu duniani na kufilisika hadi kukosa sehemu ya kulala

Tony Atlas kutoka kuwa mcheza mieleka maarufu duniani na kufilisika hadi kukosa sehemu ya kulala

Mejasoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
298
Reaction score
600
Tony Atlas kutoka kuwa mcheza mieleka maarufu duniani na kufilisika hadi kukosa sehemu ya kulala, Jamaa alikua ni kati ya wacheza mieleka (wrestlers) wakubwa duniani na akatengeneza pesa nyingi ghafla ukaanza mgogoro kati yake na mke wake Joyce White aliyeishi nae miaka 24 na kupeana talaka, Baada ya talaka mke akachukua mgao wake wa mali, Tony Atlas akabaki na kiasi kingine lakini bila tahadhari akamuamini sana rafiki yake mmoja huyo rafiki yake alimsaliti Tony na akamtapeli kila kitu alicho nacho na jamaa akabaki hana chochote hana ulinzi, nyumba wala pesa.

Akaishia kushiriki kwenye mashindano madogo ya mieleka mtaani huko massachusetts(USA) yanayoitwa ICW/IWCCW (International World Class Championship Wrestling) akawa anatengeneza pesa kidogo tu ila promotion ya mashindano hayo yalifungwa jamaa akabaki hana kazi na kuishiwa hadi akawa hana makazi tena, hana sehemu ya kulala na siku inaisha hajala chochote.

Siku moja ilikua ni siku ya baridi kali hadi barafu zinaanguka mwanamke mmoja akamuona Tony Atlas kalala kwenye bench pembeni ya bustani moja, yule mwanamke akamuonea huruma akamwambia anataka kumsaidia lakini Tony akakataa msaada, ila kwa baridi ile akaona anaweza hata kuganda na akafa mwisho akakubali msaada akaenda nyumbani kwa yule mwanamke, yule mwanamke akagundua jamaa anahitaji msaada zaidi basi akampa makazi ya muda akaanza kuishi pale, baada ya wiki kadhaa akaanza kwenda Gym kurudisha mwili wake.

Siku moja akakutana na polisi mmoja ambae alimtambua Tony kuwa alikua ni mcheza mieleka siku za nyuma yule polisi akampigia simu Vince Macmahon(tajiri maarufu kwenye WWE picha yake naiweka hapo chini) na Tonny akapata kazi WWF kwa sasa inaitwa WWE Tonny akarudi kwenye mieleka kwa jina jipya akajiita Saba Simba.

Akaanza kupata malipo mazuri lakini kila malipo akipokea basi akawa anatuma $500 sawa na Tsh 1,317,081 million moja laki tatu kwa yule mwanamke aliemsaidia kama kulipa fadhila, lakini baadae muda wake kwenye mieleka uliisha na akarudi tena nyumbani kwa yule mama, yule mwanamke akampa Tony kiasi chote cha pesa alichokua anamtumia kumbe yule mwanamke aliamua kumtunzia jamaa fedha zake, akamshauri atumie pesa hizo kutafuta leseni ya ukufunzi wa mieleka (personal trainer), jamaa akafata ushauri baadae akapata kazi WCW(world championship Wrestling).

Mwanamke aliyemsaidia Tony Atlas katika kipindi kigumu anaitwa Monica na kwa sasa amekua mke wake.


IMG-20241221-WA0031.jpg
 
Back
Top Bottom