Too much of something is indeed harmful!!

Heart

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
2,673
Reaction score
1,710
Wapendwa wana JF..katika kuchagua mwenzi kila mtu ana criterias zake.Lakini inatakiwa ikumbukwe kwamba si lazima utakutana na ambae yupo totally perfect..hakuna mwanadamu kamili..ila baadhi yetu tumekuwa too selective jamani nikianza na sisi akina dada utamsikia mmoja " Loh! ule mpua ntaupeleka wapi? mwanangu si atatisha."..

mwingine "Kha! ufupi ule jaamani,kwakweli nehi!" au utasikia "mmh,hapana mtu mwenyewe ananilazimiishaa wakati nimemwambia mie bado bado kwanza" nakadhalika.....akina kaka sasa utasikia "demu hana hata makeke,analiaaa" mwingine utasikia " bado bado,ndo naendelea kuwachambua nimebakiwa na top 5 sasa" nakadhalika..

My point is unapochagua sana napo,mwisho unachagua vibovu... Ni kweli kila mtu ana criterias zake lakini tukisema tutafute mtu perfect mmmmh! mtihani.... mwisho wadada tunakuwa hatuolewi na kuishia kuwa manungayembe wezi wa waume za watu..na wakaka kuishia kuwa gusa unase kila shimo kungia... ni hayo tu..

Jumatano njema wana JF!!
 

hahahaaa, eti huyo sio type yangu..
 
yalishakukuta nini dadaangu..!?

hamnaa hayajinikuta ila si naona...nina dada zangu wakubwa tu hawajaolewa til now sababu ya mambo hayo,wanahudhuria harusi za wadogo zao tu..
 
Kweli wanao chagua wanaishia bila kuolewa na kwakujifanya kwao kujua matokeo yao wanazeekea nyumbani au kuolewa na mke wa pili.
 
Kweli wanao chagua wanaishia bila kuolewa na kwakujifanya kwao kujua matokeo yao wanazeekea nyumbani au kuolewa na mke wa pili.

Kabisaaa dia..ndo hapo msemo wa kuchamba kwingi unapo-apply.......
 
Tatizo watu wengi wanawake kwa wanaume wanakuwa wamebezi sana kwenye outluki ya mtu,anafananaje,msomi,ana pesa,presentabo,n.k,
Wakati hivyo vitu havina mchango wowote kwenye mapnz na ni vitu ambavyo vinatengenezeka tu maishain humu,
Wengi wanaochagua chagua,wanaishia kuwa mabachela,single parents,nk na kujikuta wanazeekapeke yao,
Achen hizo jaman,km upendo upo oaneni tu pesa,unadhifu na elimu mbona vinapatikana tu mbele ya safari mkiamua!
 

Lugha gongana kuna kosa dogo na tuwekane sawa.

Hakuna neno criterias. Criteria ni wingi wa neno criterion. Vinginevyo tumia maneno ya kiswahili Kigezo (umoja) au vigezo (wingi).

Asili ya neno hilo ni Kigiriki "kritērion"
 
Kwahiyo watu wasombe sombe tu kisa ndoa itangazwe?
 
Kwahiyo watu wasombe sombe tu kisa ndoa itangazwe?

Walaaa,thats not wat i meant lizzy....suala sio kusomba somba,ila watu wasipende kutafuta vigezo vingi kana kwamba huyo mtu atamuumba mwenyewe while kuna vitu vya msingi vya kutazamia..!
 
Lugha gongana kuna kosa dogo na tuwekane sawa.

Hakuna neno criterias. Criteria ni wingi wa neno criterion. Vinginevyo tumia maneno ya kiswahili Kigezo (umoja) au vigezo (wingi).

Asili ya neno hilo ni Kigiriki "kritērion"

Oh! Thaaank yu kwa tution ndogo...haitojirudia hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…