Michael jackson anajitambulisha tu kwa staili za kipekee ambazo hazina ugumu wowote. Hiyo moonwalk ni simple kama maji, anti-gravity lean ilikuwa supporte with wires wakati inashootiwa kwenye smooth criminal na ikaja kusaidiwa na vile viatu ambavyo vilitengenezwa maalum kunasa kwenye misumari iliyotengenezwa kwa stage ili aweze kuiperfom live. Tukiachana na hapo mj hana kitu kingine cha ajabu zaidi ya kuwa na uwezo wa kucheza kwa muda mrefu bila kuchoka haraka.
Mj ni legend na kwangu ni mwanamziki namba moja ninayemkubali. Namkubali kwenye utunzi, ubunifu wa video, utundu wa kucheza na sauti ila kwenye kucheza alikuwa vizuri sana ila kuwekwa namba moja hapo siafiki sana. Labda kwasababu ni legend.