Top 20 most developed countries in Africa in 2018

Top 20 most developed countries in Africa in 2018

Hata nyie mnarasilimali nyingi kuliko Mauritius na Seychelles lakini mnapumilia mashine tu
Lol! Nope. Hivyo ni vinchi vidogo ambavyo havihitaji rasilimali nyingi sana kuendesha kama Kenya.
Kenya ina watu wengi, hivyo ingawa ina rasilimali kubwa kushinda visiwa hivyo, kamwe havitoshi kukidhi mahitaji yote ya kimaendeleo. Tanzania kwa upande wake ina ukwasi mkubwa mno wa raslimali nchi, lakini changamoto yamekuwa ukosekano wa mipango mema, siasa mbovu, na sera za kisiasa na kiuchumi ya miaka ya hapo awali ambazo hazikufaa.
 
Afrika bara lenye umaskini sana, halafu itokee nchi yako inakosa kuwepo ndani 20 bora Afrika halafu unakesha humu ukitupatia blah blah basi umerogwa. Wale jamaa wa Lumumba street mambo kama haya huyapita kimya.
Acha tu.
 
Lakini Tanzania ina population ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa nchi yenyewe. Tanzania ni kubwa hata zaidi ya Nigeria! Kiukweli.

Halafu, sio kweli ya kwamba Nigeria na Ethiopia tu ndio zimezidi Tanzania kwa idadi ya watu. DRC, SA, Egypt zina watu wengi kushinda TZ.
Kama ilivyo kwenye maandishi nakubaliana na wewe ingawa bado naamini nilichokisema, ukweli ni kwamba idadi ya watu Tanzania ilichakachuliwa wakati wa sensa ya mwaka 2012 kwa sababu wanaotoa misaada walitoa masharti ya nchi kudhibiti ongezeko la watu. Suala la ukubwa wa nchi kulinganisha na population ni kweli, bado nchi ni kubwa sana kulinganisha na idadi ya watu...
 
Back
Top Bottom