Top 5 ya wasanii matajiri Africa, Diamond Hayupo. Why?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mimi sio shabiki wa mambo ya muziki wa Tanzania, ila napenda sana kuingia mitandaoni na sifa anazopewa Diamond ni nyingi sana.

Ila nimejiuliza, baada ya pitapita zangu nimekutana jarida maarufu Marekani la Forbes limetaja wasanii matajiri zaidi Barani Africa ila cha kushangaza Diamond sijamuona kabisa, shida nini?

Nikaendelea kucheki hadi Top-Ten jamaa hayupo ila Wizkid & Davido wapo. Au uwa ni kiki tu na maisha ya kuigiza?
 

ambao ni kina nani........?...
 
Umeshindwa kuwauliza???
 
Hiyo list itakuwa na wanigeria wengi bila shaka, hawa wana fanbase kubwa na muziki wao ulipenya muda mrefu kabla yetu.

Kama utakumbuka wakati Diamond anatoka ni wimbo aliofanyiwa featuring na Davido ndo ulimpaisha so hawa walikuwa mbele kitambo.

Yote kwa yote kijana huyu wa mbagala ana mkwanja usio na mashaka hasa kutokana na kazi zake za muziki. Akiendelea kwa kasi hii ataweza ingia top5 hiyo unayoisemea.

Na hii siyo story za vijiweni sote tunaona anavyomiliki na aina ya maisha aliyonayo.
 
Tangu lini mtu anye gezea kwa watu akawa #1
 
Ni mtu asie na ubongo tu ambae anaweza kubisha kuwa diamond platnumz ana mkwanja mrefu katika wasanii hapa EA,iko wazi sasa hao forbes wako USA wanajua nini wale,wanaendeshwa na mihemko tu na ndio maana siku hizi watu wana walaumu kuwa wanapokea rushwa kuwapa kiki baadhi ya mastaa mfano kyler Jenner mdogo wa Kim Kardashian nk.

Sisi tunaomuona diamond ndio tunajua ukweli kuliko hao forbes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…