2. Sunday Manara-First ever Tanzanian footballer to play professional in Europe.
HAPO UMESAHAU KITU MKUU,
LEKEBISHA USEMI WAKO HAPO..........
KUNA MTU ANAITWA ATHUMAN ABDALLAH CHINA (Ile namba 8 ya Yanga ) alisumbua mno na yeye alienda kucheza professional Uingeleza UK. 1992 mpaka wazungu wakamfananisha na ile namba 8 yao KIPENZI CHAO MIchael Gassikoin GAZA.
ukitaka zaidi juu ya huyu jamaa na hii tri yake na kushindwa kwake just PM me na nitakutumia story nzima.
ILA LET IT BE NOTED
Vipaji tulikua navvo
Wananchi,
Tunapozungumzia vipaji vya kukumbukwa vya wacheza mpira wa miguu, ingefaa sana tukumbuke kwanza tulikotokea katika mchezo huu.
Wakati East African Challenge Cup ilipoanza, wakati huo ikiitwa Mashindano ya Gossage Cup, ubingwa ulikuwa ni wa Uganda zaidi na wenzao Kenya. Tanganyika na Zanzibar zilikuwa wasindikizaji tu.
Lakini, ilipofikia 1949 wasindikizaji Tanganyika, waligeuza kibao wakawa washindi wa Gossage Cup, watu wakafikiri labda ile ilikuwa nyota ya jaa. Hawa wazee, siku hizo vijana, wakahakikisha umahiri wao kabumbu, kwa kukichukua kikombe hicho cha mashindano ya Afrika Mashariki 1950 na 1951.
Mara tatu mfululizo. Rekodi yao hiyo haijafikiwa au kupitwa na timu nyingine yoyote ya Tanganyika wala Tanzania.
Napenda kuwapa wao heshima hiyo ya wachezaji bora wa wachezaji wetu bora:
1. Abdulhamid Ramadhani "Ibraq" - Dar Young Africans - Goalkeeper.
2. Juma Mrisho - Tabora - Fullback Right
3. Mganga Yaga - Kondoa, Dodoma - Fullback Left
4. Mambo Mzinga "Tractor" - Dar Young Africans - Halfback Right
5. Yunge Mwanansali - Tabora - Centre Half
6. Kheri Kilanga - Dar Sunderland (Simba) - Halfback Left
7. Hamisi Mtoto - Dar Young Africans - Right wing
8. Fidelis....?.... - Bukoba - Inside Right
9. Juma Abdallah Nyongole - Iringa - Centre Forward
10. William Nasson - Dar Sunderland (Simba) - Inside Left
11. Pius....?..... - Bukoba - Left wing
Reserves:
12. Mohammed Kembo - Tanga
13. Harold Mgone - Dar Sunderland (Simba)
14. Hamisi "Fourteen" - Dar Sunderland (Simba)
15. Situmai Mzee "Ng'anda" - Dar Young Africans.
Hatutawatendea haki watu hawa kama tutawasahau. Wao ndio waliotuonjesha ushindi wa mchezo huu kwa mara ya kwanza kabisa, katika mashindano ya Kimataifa.
Mwenyezi Mungu awarehemu huko waliko.