Hamna kitu...
Kuna wengine wanataja tu list ya wachezaji, ukweli ni kwamba walikuwa very average.
Mimi sikuwaona wa 70s au early 80s. Lakini late 80s kuendelea baado baado sana.
mchezaji ambaye nashangaa hakumake ni Edibily Lunyamila. That guy was something else. That guy was skillful and fast na anacheza kwenye chaki. Wachezaji wa mguu wa kushoto na skillful ni wachache...the guy was something else. Kama kuna mtu anamkumbuka mchezaji wa zamani wa Ajax anaitwa Bryan Roy...Edibily was def. on the same level.
Hussein Marsha alikuwa very skillfull na pasi za uhakika, ila alikuwa mvivu na bitozi...
Mtu kumuweka mchezaji kama Mwakalebela kwenye top defenders ni tusi.....jamaa alikuwa mbovu, sifa yake ni kukata buti za kulala tu.
George Masatu alikuwa mkali, tatizo alikuwa light-weight kama defender. The guy would get bullied.....same thing na kina Hamza Mponda (fikiria mchezaji anakunywa gongo).
Fumo alikuwa na mishuti tu, 9 out of 10 shots zinaenda jukwaani, ila akiupatia kudadeki.
hawa ni wachezaji sikukosa kuwaona kila jumamosi where possible. Wachezaji hawa ndo waliokuja kucheza timu ya Taifa na Simba na Yanga....meaning wa kina Raphael Paul, Athumani China level ile ile, inconsistent.
Wachezaji walikuwa hawana ambition kabisa.....Kitwana Selemani akipanda kwenye gari ya sponsor mwarabu akaweka kishoka na kuzungushwa mjini ndo kamaliza. Wachezaji kwenda uarabuni au Malaysia ndio wametoka.
Look, if Athumani China was so good, why didnt he make it at Reading??
Kumwita Paul Rwechungura golikipa mkali ni tusi, the guy was overweight.......
Ken Mkapa was a bully (no brains) ndo maana akaitwa "Kaburu", au "Mzee wa Kiminyio", "Bruce Lee" etc...the name says alot.
Wale mlio shuhudia mpira wa 70s kama kina FM ES, mtatudanganya kwavile hatujui tu......
Mchezaji akiwa skillful, tunaona skill tuu bila kuona uzuri wake as a Team Player......ndio mambo ya kina Malota Soma "Ball Juggler".....c'mon man. We may have skillful players but we are not team players. Au mchezaji anapiga chenga sehemu asiyotakiwa kupiga chenga....au kanzu, ili mradi watu washabikie.
Kitu kingine kilichochangia kuwasifia hawa, ni utegemezi wa kusikiliza watangazaji redioni.......wana exaggerate vitu. Ukitaka ujue uongo wao ni sawa sawa na leo hii uangalie mpira wa South America halafu usikilize watangazaji wanavyopiga makelele.......