Hili ni jambo ambalo limenitatiza sana na ni vema umeeliza swali hili. Kwa maoni yangu, Greetings and parts of the body haina maana sana, ingawa wasomi wengi watanipinga. Naamini ulisoma kingereza shuleni, sijui silabasi ya TZ iko vipi. Ningependa waTZ wanieleze. Hapa Kenya, Darasa la kwanza wanaanza na Greetings, halafu home, school, parts of the body na kadhalika kwa darasa la kwanza. Lakini katika shule za chekechea, huwa wanaanza na Phonics. Kwa maoni yangu, ni vyema uanze na Phonics (Jinsi ya kusoma Kiingereza.) Kama MTZ, kingereza utakijua kupitia Kusoma...kwa hivyo ni vyema ujue Kudecode English words. Kwa mfano, neno Tide, Swipe, na Wipe zina long vowel (I). Kwa hivyo, unaweza kusoma neno Shike (Sha-i-k), hata kama hujawahi liona. Ukisha zielewa hizo 44 phonemes na over 70 ways in which they can be written, basi unaweza anza kwa ku google 100 words Kwa kuzielewa hizo words kwa ufasaha, utaweza kusoma zaidi asilimia hamsini ya maneno yote ya kiingereza yaliyo katika maandishi.
Most common words in English - Wikipedia, the free encyclopedia
Hivi sasa, naandika kitabu cha kiingereza cha darasa la kwanza hapa Kenya, na jambo hili linanitoa jasho sana.
Kwa hoja nyingine; unaweza kujua jinsi naweza pata vitabu vya darasa la kwanza vya TZ. Asante