Leo twitani kumechafuka na picha ya mtu anayeteswa kwa kuning’ining’zwa kama mshikaki.Ni jambo la kuhuzunisha sana.
Naomba nihitilafiane na wengi ambao wamekilaani kitendo hiki ingawa nami sikiungi mkono ila kwa masharti.
Mahakamani kuna mtu kaelezea alivyoteswa na askari Polisi nami nakubaliana na askari kutumia mateso kama njia ya kupata habari ambayo inaweza kusaidia kuokoa maisha ya wengi.Hili linafanyika nchi nyingi na watu kama wamarekani wanaita “enhanced interrogation” ambapo yamo hata yale mateso maarufu ya “water boarding”.
Tofauti na wenzetu ambao hukusanya taarifa na kumhoji mtuhumiwa kwa muda mrefu na kujiridhisha kuwa kuna habari inafichwa, kwetu sisi kama ilivyosemekana mahakamani within hours mtu keshapelekwa katika mateso makubwa na ya ajabu.Hakuhojiwa hata na wapelelezi tofauti na kisha ku triangulate information ili kujua palipo na wingu.Ni kukamata na kumpeleka mtu katika mateso makubwa.Jambo la pili ni ukubwa wa kosa,kama waliopitia mikononi mwa Polisi wataamua kufunguka kuna watu ambao makosa yao ni madogo sana lakini walikiona cha moto.
Napendekeza PGO iwekewe kipengere cha “enhanced interrogation” na utaratibu uwekwe wazi ili ijulikane ni nani anayestahili kuamrisha haya yafanyike na kwa kosa gani.Isiwe kila askari ana uwezo na mamlaka hayo.
Naamini kuna mahali mateso haya yamesaidia hasa katika kupata silaha zilizotumika katika matukio lakini pia kuna uwezekano kuna watu wamepitia jahanamu hii bila kuwa na hatia.Marais wetu wanaogopa kusaini adhabu ya kifo kwa hofu hii kuu ya uwezekano wa kumyonga mtu asiye na kosa.
Ni UWELEDI versus MABAVU!!
Sasa wewe mkubwa unaposema;
"...napendekeza PGO iwekewe kipengere cha 'enhanced interrogation' na utaratibu uwekwe wazi..."
Wewe unaijua na umewahi kuisoma PGO achilia kwanza kuielewa...?
Wewe unadhani jambo hili muhimu na maelekezo yake ya namna ya kulitekeleza linaweza kukosekana kwenye utaratibu wa polisi wa kila siku wa kutekeleza majukumu yao as stipulated in the PGO...?
SIKILIZA NDUGU YANGU NA WENGINE WOTE MNAONISOMA HAPA;
##Tatizo hapa siyo PGO...
##Tatizo hapa siyo sheria zinazoongoza utendaji kazi wa jeshi la polisi....
##Tatizo hapa siyo Polisi mwenyewe kama watu...
å Tatizo letu hapa ni MFUMO MBAYA WA UTAWALA unaotoa IMPUNITY kwa viongozi (watawala) wasiowajibika kwa YEYOTE kwa maamuzi yao kiasi cha kujiona wako juu ya SHERIA...!!
##Na kwa kesi hii inayoendelea, tatizo siyo watuhumiwa kuteswa ili polisi kupata taarifa muhimu za kiusalama na upelelezi ili kuzuia maafa...
##Tatizo la polisi na waendesha mashitaka kwenye kesi hii ya Freeman Mbowe na wenzake ni msingi wa mashitaka yenyewe kuwa ni UONGO wenye HILA ndani yake kwa kuwa tu watawala wenye IMPUNITY wanataka kumtoa ktk picha mtu fulani aliye kikwazo cha maslahi yao binafsi...
Udhaifu huu wa polisi katika hoja ya hapo 👆👆👆 juu ndiyo ambayo mawakili wa upande wa utetezi wanajaribu kuuweka wazi kwetu na kutufanya kuliona Jeshi la polisi ktk picha yake halisi...
Ndiyo maana, polisi wote (akiwemo RPC wa Kinondoni ACP Ramadhani Kingai kama mbeba mikoba wa kesi) waliokwisha kutoa ushahidi, wamedhihirisha wazi kuwa hawana uelewa na sheria, kanuni na miongozo ya utendaji kazi wao wa siku kwa siku unaojulikana kwa jina la "POLICE GENERAL ORDERS - PGO"...
##Kwa hiyo, kwa kuwa msingi wa kesi yenye ni UONGO, kamwe hawawezi kutumia njia halali mbele ya macho ya sheria kutafuta au kukusanya ushahidi wao...
##Kwa hiyo ndugu kama ni watuhumiwa kuteswa na kutwezwa utu wao kwa njia isivyo halali, imefanyika si kwa sababu hakuna sheria na utaratibu wa kisheria unaowaongoza polisi kukusanya ushahidi wao kwa kutumia njia zote ikiwemo hiyo ya "kutesa au - enhanced interrogation", bali ni kwa sababu ya IMPUNITY isiyo rasmi wàliyo nayo ambayo huwasukuma kutekeleza for their self & personal interest badala ya public interests....!!