Torture (Kutesa)

Ma.p.u.mbu yako wewe, maharamia wakubwa nyie. Dawa yenu inachemka, vuteni subra
 
Mkuu toa neno la laana kwa hawa jamaa usipite hivi hivi
 
nchi watu wake wenye utamaduni wa kupendana na kuishi kwa aman na furaha.
lakini serkali inatengeneza matatizo yenyewe ..!!!!
 
Kutesa siyo njia sahihi ya kupata ukweli. Mfano, ukimtesa mtu ambaye hajui kitu kuhusu habari unayotaka au unayoitafuta utapata ukweli gani? Kwa hiyo, kuna mambo mawili: 1) unaweza ukamtesa na ukapata ukweli na 2) unaweza kumtesa mtu na usipate ukweli (kwa mfano kama kesi ni ya kupika). Kwenye haki jinai kuna kanuni inayosema 'better that 10 guilty persons escape, than that one innocent suffer' ambayo msingi wake unatoka kwenye Kitabu cha Kutoka (Genesis) 18:21-32. Benjamin Franklin, mmoja wa waanzilishi wa taifa la Marekani aliwahi kusema "it is better a hundred guilty persons to escape than one innocent person to suffer.” Kwa hiyo, mateso siyo njia sahihi ya kupata habari kuhusu tukio fulani na mahakamani jaji au hakimu akijiridhisha kuwa shahidi alisema uwongo (kwa kukiri alichotakiwa kusema na watesi wake) atatupilia mbali ushahidi wa Jamhuri dhidi yake. Ila kama kuna ushahidi kwamba mtuhumiwa alitenda uhalifu na katika kuteswa akakiri, then kuteswa kwa mtuhumiwa hakuwezi kumsaidia maana hata kama asingeteswa ushahidi bado ungejitosheleza (ungesimama) na jaji au hakimu akijiridhisha hivyo, basi atamtia mtuhumiwa hatiani licha ya kwamba aliteswa ili akiri kushiriki kwake kwenye uhalifu.
 
siku ukichomwa bisibisi matakoni utajua zaidi torture ninzuri kissing gani
 
Sasa wewe mkubwa unaposema;

"...napendekeza PGO iwekewe kipengere cha 'enhanced interrogation' na utaratibu uwekwe wazi..."

Wewe unaijua na umewahi kuisoma PGO achilia kwanza kuielewa...?

Wewe unadhani jambo hili muhimu na maelekezo yake ya namna ya kulitekeleza linaweza kukosekana kwenye utaratibu wa polisi wa kila siku wa kutekeleza majukumu yao as stipulated in the PGO...?

SIKILIZA NDUGU YANGU NA WENGINE WOTE MNAONISOMA HAPA;

##Tatizo hapa siyo PGO...

##Tatizo hapa siyo sheria zinazoongoza utendaji kazi wa jeshi la polisi....

##Tatizo hapa siyo Polisi mwenyewe kama watu...

å Tatizo letu hapa ni MFUMO MBAYA WA UTAWALA unaotoa IMPUNITY kwa viongozi (watawala) wasiowajibika kwa YEYOTE kwa maamuzi yao kiasi cha kujiona wako juu ya SHERIA...!!

##Na kwa kesi hii inayoendelea, tatizo siyo watuhumiwa kuteswa ili polisi kupata taarifa muhimu za kiusalama na upelelezi ili kuzuia maafa...

##Tatizo la polisi na waendesha mashitaka kwenye kesi hii ya Freeman Mbowe na wenzake ni msingi wa mashitaka yenyewe kuwa ni UONGO wenye HILA ndani yake kwa kuwa tu watawala wenye IMPUNITY wanataka kumtoa ktk picha mtu fulani aliye kikwazo cha maslahi yao binafsi...

Udhaifu huu wa polisi katika hoja ya hapo 👆👆👆 juu ndiyo ambayo mawakili wa upande wa utetezi wanajaribu kuuweka wazi kwetu na kutufanya kuliona Jeshi la polisi ktk picha yake halisi...

Ndiyo maana, polisi wote (akiwemo RPC wa Kinondoni ACP Ramadhani Kingai kama mbeba mikoba wa kesi) waliokwisha kutoa ushahidi, wamedhihirisha wazi kuwa hawana uelewa na sheria, kanuni na miongozo ya utendaji kazi wao wa siku kwa siku unaojulikana kwa jina la "POLICE GENERAL ORDERS - PGO"...

##Kwa hiyo, kwa kuwa msingi wa kesi yenye ni UONGO, kamwe hawawezi kutumia njia halali mbele ya macho ya sheria kutafuta au kukusanya ushahidi wao...

##Kwa hiyo ndugu kama ni watuhumiwa kuteswa na kutwezwa utu wao kwa njia isivyo halali, imefanyika si kwa sababu hakuna sheria na utaratibu wa kisheria unaowaongoza polisi kukusanya ushahidi wao kwa kutumia njia zote ikiwemo hiyo ya "kutesa au - enhanced interrogation", bali ni kwa sababu ya IMPUNITY isiyo rasmi wàliyo nayo ambayo huwasukuma kutekeleza for their self & personal interest badala ya public interests....!!
 
Well said.
 
Ma.p.u.mbu yako wewe, maharamia wakubwa nyie. Dawa yenu inachemka, vuteni subra
Nashukuru kwa matusi yako lakini kwa unafiki wa watanzania nyie ndio mnaomtoa mtu roho kwa kukwapua simu ya shillingi laki moja.Ukimpiga tofali mwizi wa simu unaona raha,pambafuuu
 
Ebu tuseme ukweli tu je kumtesa mtu kwa maslahi ya watu fulani au chama fulani hasa kwa maslahi ya viongozi ni sifa? Halafu hata hizo njia unazosema kwamba hata marekani inazitumia hapa juzi tu walisema ilikuwa inakiuka utu na haki za binadamu, Kwa uzoefu inaonyesha polisi wa tanzania ni wazuri sana kwenye utesaji, ila kwa nchi zilizoendlea kitu kama hicho kikitokea na baadae ikaonekana kuna uonevu ulifanyika juu ya mtuhumiwa serikali huwa inatoka na kusema ukweli na hata kulipa fidia je vip kwa nchi yako ya tanzania? Ukweli ni kwamba siku jeshi la polisi likiacha kupokea maelekezo kutoka juu na kila polisi anaefanya tofauti ni PGO yao kuwajibishwa ndo tutajua kuna weledi katika jeshi hili, ila kwa sasa jeshi la polisi linahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo na pia jeshi la polisi liachwe liwe huru bila kuingiliwa na serikali na wana siasa
 
ndio maana unaambiwa jiepushe na uhalifu,kama huna namna ukishikwa nyoosha maelezo.
mambo ya kujaribu vifua vya watu,ni kupimana imani kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…