Total energies hii sio sawa kabisa

Chujio

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2013
Posts
1,368
Reaction score
2,108
Habari wadau, haya ni malalamiko yangu juu ya vituo vya kujazia mafuta vya kampuni husika.

Hivi karibuni walianzisha mfumo wa kadi ambayo unaweka deposit ya pesa kadhaa na kukuwezesha kuitumia unapolazimika kuweka mafuta lakini cha kushangaza sasa, vituo vyenyewe vimekuwa bila mafuta na kulazimisha mteja kutumia pesa ya ziada kuweka mafuta kutuo kingine na kutuingizia hasara

Hii ni siku ya pili sasa vituo havina mafuta kabisa, ukienda unaambiwa upite tu vile hawana kitu. Uaminifu na accountability ni sifuri kabisa, I am very disappointed.

Kama shida ipo itatuliwe haraka, la sivyo hapakuwa na haja ya kuruhusu watu tujicommit kuwa na kadi ilihali vituo havina mafuta na watu kuingia hasara. Au refund kwa wateja wao

Kutoka kwa mteja mkereketwa
 
We kwann uchukue kadi kiongozi tuanze na hapo
Ndio hii hasara kwa wenye kadi, kwamba unaweka pesa yako ya mafuta kwenye mfumo wao wa malipo (prepaid) lakini kwa masikitiko, vituo havina mafuta. Hiyo kadi haina msaada wowote, afadhali ukabaki na kash yako ukawekea sehemu nyingine yebye mafuta
 
WANAKERA SANA SANA HAWA JAMAA!YAANI WASHANICOST SANA HII ISHU YAOO YA KUKOSA MAFUTAA!!!
 
Mfumo wa malipo kabla ya huduma hauja kaa sawa huku bongo, labda kwenye hii mitandao ya simu.
Lakini kwa usalama na kutofikwa kadhia kama hizo heri uwe na hela yako ukienda hapa hamna mafuta unaenda pale.
 
WANAKERA SANA SANA HAWA JAMAA!YAANI WASHANICOST SANA HII ISHU YAOO YA KUKOSA MAFUTAA!!!
Asante mkereketwa mwenzangu, ni kwamba tu hii prepeaid service yao ni wazo zuri lakini utekelezaji wake sifuri kabisa. Wameshindwa kuwa reliable kwenye huduma hii
 
Mfumo wa malipo kabla ya huduma hauja kaa sawa huku bongo, labda kwenye hii mitandao ya simu.
Lakini kwa usalama na kutofikwa kadhia kama hizo heri uwe na hela yako ukienda hapa hamna mafuta unaenda pale.
Ni kweli kabisa, mara nyingine hata malipo kwa mtandao unasumbua. Tutafika lakini. Majirani zetu wapo vizuri sana kwenye ishu ya kuwa cashless
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…