Tottenham Hotspurs Thread

Pongezi kwa Mourinho kwa kwenda naye taratibu mpaka amekuwa na full fitness.
Anyway, siku ile jamaa mbeya city spurs nilikua namuambia Bale anatakiwa aanze akasema siyo performer mzuri. Nilisema ukimuweka Bale, Son, Ndombele na Kane hiyo game moto unawaka.

Jose kabadili formation kampa chance Bale matunda anayaona.

Nasikia anatishiwa kufukuzwa
 
Mnamuona Bale akianza?
Haikuwa kazi rahisi kumfanya acheze hivi. Amecheza vizuri mechi 3 mfululizo ndiyo sababu alistahili kuanza leo na ameweka furaha kwa kila shabiki wa Spurs. Sasa huenda tumetatua tatizo la RW.

Leo timu ilikuwa na balance kila idara hivyo kila mchezaji kapafom. Sonny alikuwa [emoji91][emoji91][emoji91].

Huyu ndiye Bale tunayemtaka siyo yule wa wiki kadhaa zikizopita.

#COYS
 
Naelewa unachomaanisha mkuu. Kila mtu, na hata Mourinho kasema juzi, anataka kuona Bale kama huyu. Kuanzia game 5 zilizopita kurudi nyuma ukitazama performance ya Bale hata ungekuwa wewe ndiye kocha usingempanga. Naamini hukutazama mechi za Europa alizokuwa akipewa nafasi kuanza au kutokea benchi.
 
Pongezi kwa Mourinho kwa kwenda naye taratibu mpaka amekuwa na full fitness.
Process kama waliyoenda nayo kwa Bale ndiyo ningependa pia itumike kwa Lo Celso. Hakuna sababu ya kumharakisha. Kaanza mazoezi ila apewe dk chache kwenye mechi ndogo au pale mechi inapokuwa "imeuawa".

Natamani sana watu wangetambua nafasi ya benchi la Spurs kwenye kumfufua Bale.
 
Nimeangalia games alizoanza. Kuna double touch anazifanya ndani ya box huku akiwa anacheza dakika kumi za mwisho. Imagine aanze tangu mwanzo. This guy ni kiboko
 
Spurs iwekeze kwenye kununua wachezaji, bado haina quality ya kupigania makombe makubwa.
 
Unadhani angekuwa na quality ya leo toka awali Madrid wangemwachia?
Ronaldo alivyoachiwa alikuwa flop?

Casillas?

Navas?

Rodriguez?

Jovic?

Isco aliyemuweka benchi siku hizi ndiyo ST wake.

Ni basi tu kiburi cha makocha.
 
Nimeangalia games alizoanza. Kuna double touch anazifanya ndani ya box huku akiwa anacheza dakika kumi za mwisho. Imagine aanze tangu mwanzo. This guy ni kiboko
Suala la fitness yake umelizingatia kweli. Hakuwa na uwezo hata wa kumaliza dk 60. Tangu msimu auanze kawa majeruhi angalau mara tatu. Hivyo process ilikuwa inaanza upya kila baada ya mechi mbili tatu.

Bale anapendwa sana na kila mtu pale Spurs. Na huyo kocha ndiye aliyeanza kumtaka akiwa Madrid. Ni kwamba tu Levy alikuwa mgumu biashara ikafanyika wakati wa Ancelotti. Hivyo hakuna anayembania.

All in all, ni kwamba kila shabiki wa Spurs ni mwenye furaha kwa mechi hizi 4 zilizopita. Pamoja na kufungwa na Westham, kuna wachezaji muhimu wanarejesha viwango vyao; Dele Alli na Bale.

Hivyo matatizo ya RW na CAM tuliyokuwa tukilialia hapa yatapungua sana.
 
Ronaldo alivyoachiwa alikuwa flop?

Casillas?

Navas?

Rodriguez?

Jovic?

Isco aliyemuweka benchi siku hizi ndiyo ST wake.

Ni basi tu kiburi cha makocha.
Mkuu Castr unajua inaniumiza sana kuona ukiikosa point ya suala la Bale. Huyu ni mchezaji ambaye hakupata enough game time kwenye misimu miwili iliyopita.

Pia aliandamwa sana na majeruhi madogo madogo ya mara kwa mara. Juzi Jose kaelezea kwa nini majeraha madogo madogo ya mara kwa mara ni mabaya kuliko jeraha kubwa la mara moja. Alikuwa akielezea process ya kurejesha form ya Dele Alli.

Suala la Bale halikuwa rahisi kihivyo. Narudia, kama kweli uliangalia display za Bale mechi zilizopita tangu msimu uanze (ukitoa hizi 4 mfululizo zilizopita) usingempanga kucheza kama ungekuwa wewe ndiye kocha.

Hakukuwa na ambition, quality na motivation kabisa. Na si Bale tu, ni kwa Dele Alli na Moura pia. Moura anayo determination ila hana quality. Hii ndiyo sababu kocha alikuwa akilazimika kumuanzisha Bergwijn kwenye RW.
 
Spurs iwekeze kwenye kununua wachezaji, bado haina quality ya kupigania makombe makubwa.
True this. Pamoja na kucheza vizuri jana kuna maeneo bado yako wazi. Mfano; jana unaweza dhani CAM alikuwa Sonny kumbe alikuwa Moura. Kwa kifupi Lo Celso huenda akashindwa kuziba pengo la Eriksen. Dele Alli auzwe tupate CAM mzuri.

Bila no 10 mzuri wote tunaona namna Kane anavyoanza kuharibika. Kapoteza sharpness kabisa. Pia anaonekana mchovu kuanzia dk ya kwanza.

Kwenye CB Toby alilazimika kucheza kushoto eneo ambalo si lake. Defensively tulikuwa salama mwanzoni mwa mchezo wakati Burnley wakiwa butu kiushambuliaji.

Walipoamka ilibidi kumchezesha Hojbjerg katikati ya CBs wetu ili kupata clean sheet.
 
Hii timu yule mjinga Levy akitupatia walau wachezaji watatu tu summer tunakuwa contenders wa vikombe vyote msimu ujao;

1. Left sided CB kuziba pengo la Jan Vertonghen. Hapa sitashangaa wakitelezea ganda la ndizi kwa Sergio Ramos on free transfer. Ramos atakuwa starter na back up zake Eric Dier na Joe Rodon.

2. Namba 8 mzuri. Tunahitaji kiungo mkabaji mchezeshaji mzuri atakayekuwa akimpa changamoto Ndombele kwenye midfield duo au akim-complement kwenye midfield trio. Nazungumzia mchezaji kama Marcel Sabitzer.

3. Namba 10. Tunahitaji mshambuliaji mchezeshaji akazibe pengo la Eriksen. Lo Celso ni injury prone na kakosa pre-season mbili zilizopita hivyo suala la kumjengea fitness limekuwa gumu na halihitaji haraka. Dele Alli auzwe.

Hapo hakuna timu itataka kucheza na sisi.
 
Hoja inaungwa mkono, ila nina wasiwasi na biashara za Levy, ana biashara ngumu sana anaweza kuleta watoto wa academy ili waje wachipukie.
 
Hoja inaungwa mkono, ila nina wasiwasi na biashara za Levy, ana biashara ngumu sana anaweza kuleta watoto wa academy ili waje wachipukie.
[emoji817]. Aiseee, yule bwana biashara zake ni tatizo. Katika makinda wote tulionao ni wawili tu wanapaswa kuwepo kikosi cha kwanza kwa mwenendo wa kocha.

Kuna dogo holding midfielder anaitwa Oliver Skipp. Yuko kwa mkopo Norwich City. Dogo ndiyo future ya timu na replica ya Hojbjerg.

Pia kuna yule dogo striker anaitwa Lavinier. Yule aliyetoa assist kwa Bale kwenye game ya Europa. Sasa Levy na mambo yake ya kiingereza ataanza kulazimisha madogo wasio na vipaji kama akina Troy Parrot wabaki badala ya kuwauza kwa vitimu vidogo.

Nakumbuka msimu uliopita namna walivyomwekea presha Jose amkubali Troy Parrot kama back up ya Kane wakati dogo hamna kitu. Kocha alikomaa nusu msimu bila striker ndipo wakajua haiwezekani. Kila mara aliwaambia "He is not ready".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…