Ligi ndiyo hiyo imeisha na angalau tutacheza kombe ambalo Jose kasema kufuzu maana yake kulibeba tayari! Kacheza mara mbili na kalibeba mara hizo. Kwa maneno yake mwenyewe kasema siyo mbaya kushiriki kwa mara ya 3 na kulibeba kwa mara hiyo.
Siyo mbaya. Kipi bora? Kushiriki UCL na kuishia fainali au kushiriki UEL na kulibeba? Mafanikio hupimwa kwa vikombe na si idadi ya fainali ulizocheza.
Natarajia kutakuwa na sura mpya dirisha hili la msimu wa korona. Binafsi nadhani kuna maeneo yafuatayo yanahitaji uwekezaji.
1. CD. Hapa tuna Dier, Sanchez, Tanganga, Toby na Foyth. Super Jan anaondoka. Pia inaonesha kocha hajamkubali dogo Foyth. Eric Dier kasaini mkataba mpya kwa sharti la kucheza kama CB. Napendekeza anunuliwe CB mnyumbulifu wa kuimarisha safu ya ulinzi.
2. DM. Hapa tayari dogo Oliver Skipp kasaini mkataba wa kudumu mpaka 2024. Hata hivyo bado tunahitaji holding midfielder wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Wanyama/Dier. Hapa nadhani apatikane mkongwe wakati dogo Skipp anaendelezwa mdogo mdogo.
Kwenye DM's wanyumbulifu nadhani Sissoko angeuzwa tu. Nafasi yake ichukuliwe na Sergej Milinkovic Savic wa Lazio. Akawaongezee nguvu Ndombele, Gedson, Winks, na Lo Celso.
3. RW. Hapo Lamela atoswe tupate ingizo jipya umri na calibre ya Steven Bergwijn. Hivyo tutakuwa na Sonny/Bergwijn kwenye LW. RW tutakuwa na Moura na hilo ingizo jipya.
3. No. 10. Hapa kwenye namba 10 tunaye Lo Celso tayari ambaye kimsingi ndiye mbadala wa Eriksen. Wasiwasi wangu ni "The Dele Alli problem" kama anavyosemaga Mourinho. Dele hawezi mbenchi Lo Celso nyuma ya ST. Dele kukaa benchi kutapelekea chokochoko kutoka kwa English media. Ningekuwa Mourinho ningemuuza tu na pesa hiyo plus ile ya Lamela ningenunulia winger mzuri wa kulia.
4. FB. Suala la full backs liko wazi. Ssengnon hawezi kuwa full back karibuni. Anaweza zaidi kama wingback na Mourinho angependa full back. Hivyo ni ama auzwe Ben Davies au dogo C
Sess. Suala la kuleta mabeki wapya kulia na kushoto ni la lazima hslihitaji mjadala.
5. ST. Hapa itategemea na ikiwa Kane ataondoka au laa. Nimesikia tunamnyatia Zaniolo wa AS Roma japo kocha wao kakanusha.
Ngoja tusubiri tuone.