Tottenham Hotspurs Thread

Pia inaonesha Ndombele anaweza kwenda Inter. Wanamhitaji. Kama wakitupatia Milan Skrinial na sisi tukawa na uwezo wa kutafuta mbadala wake (Ndombele) sioni tabu. Wamchukue tu.


 
Ni furaha tu kwa shabiki wa Spurs. Usajili umepangiliwa kweli. Sasa suala la FB ni dhahili linaenda kupewa majibu. Serge Aurier a. k. a uncle kidevu anatakiwa na Milan. Tunamshukuru kwa huduma zake ila aende tu kwa maslahi ya pande zote mbili.

 

Europa Cup ni inferior cup.

Ukitafuta malengo ya timu zote kubwa utakuta ni kucheza UEFA ila siyo kuchukua Europa.

Jiulize swali, kwa nini bingwa apate ticket ya kushiriki UEFA badala ya Europa alilochukua?
 
Hatimaye suala la holding midfielder limepatiwa ufumbuzi na sasa timu ina uhakika wa kukaba inapocheza.
 
Usajili wa hii timu bado haujaeleweka, msimu ujao nadhani timu itakuwa inashiriki ila si kushindana.
Usajili unaenda poa kwa kuzingatia madhara ya covid 19 ambapo inasemekana timu itapoteza takriban £200m. Hivyo ni vema kutumia kwa tahadhari. Kununua wachezaji wazuri lakini ambao ni cheap bargains.

Mfano. Kutatua tatizo la kiungo ya ukabaji timu isingeweza kusajili mchezaji kama Ngolo Kante au Kasemiro. Lakini ikiwa wamempata want-away wa Southampton (Hojbjerg) kwa £3m + Kyle Walker Peters (£12m), huo ni usajili mzuri kuliko hata Chilwell kwa £50m.

Pia angalia tunamsajili Matt Doherty kwa £12m + add ons zisizozidi £5m. Huyu ndiye full back wa pili kwa kutengeneza nafasi ndani ya epl kwa misimu miwili iliyopita. Ni upgrade nzuri sana ya Serge Aurier kwenye namba 2.

Mkakati wa Levy kwenye dirisha hili ni one out one in. Ili ununue, lazima uuze. Naiona Spurs ikiwa mshindani wa ubingwa msimu ujao.


Washindani wa ubingwa msimu ujao:

Liverpool x City x Chelsea x Spurs.


Washindani top six finish:

United, Arsenal, Wolves, Leicester, Everton.
 
Man Utd ana kikosi kizuri kwa sasa na huenda akakiimarisha zaidi, wana nafasi ya kufanya vizuri labda mwalimu azengue kwenye mbinu, Arsenal nao wameshafanya usajili mzuri na bado hawajatosheka. Kiukweli lolote linaweza kutokea.
 
Timu inamsajili Doherty. Halafu tweets za Doherty kusema yeye ni shabiki wa Arsenal zinaibuka.

Hii timu mara ya mwisho kuchukua kombe lini?
 
Timu inamsajili Doherty. Halafu tweets za Doherty kusema yeye ni shabiki wa Arsenal zinaibuka.

Hii timu mara ya mwisho kuchukua kombe lini?
Cha ajabu nini hapo. Arsenal ni timu anayoipenda tangu utotoni. Kasajiliwa na mahasimu wao Spurs makaburi yakufukuliwa. Kazidelete tweets hadharani na sasa ni Spurs 100%. Kama unadhani kila mchezaji duniani anachezea timu yake ya moyoni basi kuna shida kubwa.




 
Mara ya mwisho kuchukua kombe lini?
 
Mmejikausha ili tuwasahau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…