Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Mourinho atamaliza mwaka pale Tottenham? Nina mashaka makubwa.Klabu ya Tottenham Hotspurs imemfuta kazi Kocha wake Mauricio Pochettino mwenye miaka 47, baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka mitano
Taarifa ya timu inasema matokeo ya mwishoni kwa ligi za ndani msimu uliopita na matokeo ya msimu huu si ya kuridhisha
Pochettino aliyeiongoza timu hiyo kufika Fainali ya Klabu Bingwa msimu uliopita, ameondoka klabuni hapo pamoja na Msaidizi wake, Jesus Perez huku Wakufunzi wengine, Miguel d'Agostino na Antoni Jimenez nao wakiondoka klabuni hapo
UPDATE
Jose Mourinho amechaguliwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspurs ya England hadi mwisho wa msimu 2023
Kocha huyo wa zamani wa Klabu za Manchester United na Chelsea za England pia anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino
******
Tottenham have sacked head coach Mauricio Pochettino after five years in charge of the Premier League club.
The former Southampton boss, 47, was appointed in May 2014 and led the club to the Champions League final last season, where they lost to Liverpool
But Spurs have made a disappointing start to the current campaign and are 14th in the Premier League.
"We were extremely reluctant to make this change," said Spurs chairman Daniel Levy.
"It is not a decision the board has taken lightly, nor in haste. Regrettably domestic results at the end of last season and beginning of this season have been extremely disappointing.
"It falls on the board to make the difficult decisions - this one made more so given the many memorable moments we have had with Mauricio and his coaching staff - but we do so in the club's best interests."
Pochettino's assistant Jesus Perez, and coaches Miguel d'Agostino and Antoni Jimenez have also left the club.
Tottenham said in a statement that they would provide an update on new coaching staff "in due course".
Pochettino guided Tottenham to the League Cup final in his first full season while two third-placed finishes sandwiched a runners-up spot in the Premier League in 2017.
UPDATES
Jose Mourinho has been named Tottenham head coach until the end of the 2023 season. The former Manchester United and Chelsea boss replaces Mauricio Pochettino, who was sacked on Tuesday.
Negotiations between Spurs and Mourinho - who had been out of work since leaving Old Trafford in December - intensified over the last few days and concluded in the early hours of Wednesday morning.
Hii ni ndiyo ya ajabu sana. Mourinho anapenda club zenye uwezo wa kutumia pesa kuwanasa mastaa anaowahitaji kwa udi na uvumba. Kinyume cha hapo inakuwa nongwa. Ilikuwa moja ya sababu ya kuondoka Man U. Hawakuweza kutimiza kila hitaji lake na yeye alichangia kusajili vimeo kadhaa.
Upande mwingine, Kiongozi wa Tottenham Daniel Levy ni Mpare wa Uingereza. Anapenda kutumia kidogo kununua wachezaji lakini aweze kuwauza pakubwa baadaye. Si mshindani kwenye soko la kununua. Ni ngumu kutoa pesa na bila shaka Mourinho atakuwa frustrated ndani ya miezi kadhaa hasa msimu wa joto wakati wa usajili.
Ili ndoa ifanye kazi, mmoja lazima akubali kufuata ya mwenzie. Ama Mourinho akubali kufanya kazi na bahili Levy au Tottenham wakubali kumwaga pesa ili wachukue kombe la EPL au Champions League. Sioni mmoja wao akikubali kirahisi kuacha misingi yake.