Tottenham yamtimua Pochettino na benchi lote la ufundi. Jose Mourinho ateuliwa kuinoa Klabu hiyo

Mourinho atamaliza mwaka pale Tottenham? Nina mashaka makubwa.

Hii ni ndiyo ya ajabu sana. Mourinho anapenda club zenye uwezo wa kutumia pesa kuwanasa mastaa anaowahitaji kwa udi na uvumba. Kinyume cha hapo inakuwa nongwa. Ilikuwa moja ya sababu ya kuondoka Man U. Hawakuweza kutimiza kila hitaji lake na yeye alichangia kusajili vimeo kadhaa.

Upande mwingine, Kiongozi wa Tottenham Daniel Levy ni Mpare wa Uingereza. Anapenda kutumia kidogo kununua wachezaji lakini aweze kuwauza pakubwa baadaye. Si mshindani kwenye soko la kununua. Ni ngumu kutoa pesa na bila shaka Mourinho atakuwa frustrated ndani ya miezi kadhaa hasa msimu wa joto wakati wa usajili.

Ili ndoa ifanye kazi, mmoja lazima akubali kufuata ya mwenzie. Ama Mourinho akubali kufanya kazi na bahili Levy au Tottenham wakubali kumwaga pesa ili wachukue kombe la EPL au Champions League. Sioni mmoja wao akikubali kirahisi kuacha misingi yake.
 
Goodluck to Morinho
Tunamsubiri Stamford bridge aje achezee kichapo
 
Kuanzia leo mie ni shabiki wa tott na united....sadly!!😔
 
Mkuu unauliza kama utawala wa Mourinho utarudi! Kwani utawala wake uliwahi kuondoka?
 
Inaonekana huwa unaota ukiwa unatembea mkuu
 
Ni nguvu ya soko na fedha ndio inamrudisha Morinyo epl ila kimpira tot inaenda kuwa ya kuweka basi tu foleni wakati wa poch walikuwa wanafunguka hadi raha
Toka Mourinho ashindwe pale OT hana jipya kwenye ulimwengu wa footbal, angeingia timu za taifa au awe mchambuz pale Sky sport tu
 
nategemea kuiona Tottenham yenye kiwango bora kabisa
 
Mourinho hawez kutua spurs sababu vision za mmiliki na yeye ni tofaut mwenye timu nahili haamini katika
Kuvunja bank kuleta mapro. Mourinho anataka timu yenye kutenga fungu lolote atakalo
wewe jamaaaa hovyo kweli
 
Ki ukweli, mi binafsi sioni makubwa kwenye Spurs ya Mourinho, kama alirudi Chelsea akazingua, Man akazingua sidhani kama Spurs atakuwa na jipya.
Man alizingua vipi wakati alichukua Europa na League Cup?
 
Nakuakikishia Ole atafanikiwa pale OT, mark my word, Ole anaitaji madirisha mawili zaidi ya usajiri kurudisha hadhi ya Man Utd
Hakuna kitu pale...debe tupu lile...sendeka ni msimamizi wa mazoez tu na kuhakikisha wachezaji wanakua wasafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…