Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Nadhani leo nimeamua nishee nanyi uzoefu wangu kuhusu kilimo. Mi nimekuwa nikilima nyanya ila kwa miezi michache iliyopita nimeanza kulima matango. Cha kushangaza matango yamekuwa ni biashara nzuri kwa wakulima wanaoluma matango. Nami pia nimeona mafanikio yake. Na ni vizuri ukitumia mbegu bora ndio utapata mafanikio unayitaka. Mbegu ninayotumia inaitwa Monalisa F1 ambayo ni ya mwezi mmoja na siku tano unavuna
 
Ningewashauri nanyi mjaribu. Kwa wale wenye formula yanfu, utatumia mwongozo ile ule ila tu ni kwa mbegu ya matango. Mbegu hii inauzwa sokoni kkoo n.sh. 5000 kwa mbegu 75

Mkuu heshima kwako,
Huu ulimaji nao unahitaji maji na mambo kadha wa kadha unaweza kunisaidia in details hapo au kama kuna link nipite mwenyewe nione namna ya kuendesha kilimo cha matango.
Natanguliza shukran sana kwako.
 
Sasa mkuu, tuambie kiukweli kati ya matango na nyanya ni kipi hutumuii mtaji mkubwa na ulipaji wake kipi zaidi
 
Naomba kujua unamaanisha formula ile ile ya nyanya?
Ungetupa maelezo ya kutosha .Vipi spacing ya matango iko vipi n.k.
 
Kwa wale wajasiriamali wanaohitaji kujiunga na group ya WhatsApp kwa masuala ya kijasiriamali nicheki 0762600100
 
Sasa mkuu, tuambie kiukweli kati ya matango na nyanya ni kipi hutumuii mtaji mkubwa na ulipaji wake kipi zaidi

Nyanya inalipa ila kwa muda mrefu. Matango yanalipa zaidi kwa kuwa ni ya muda mfupi. Zamani nilikuwa nalima nyanya pekee ila nilipoanza na matango, matango yanalipa zaidi hivyo nawashauei watu walime matango pia hayanywi maji ka nyanya
 
Unapata tango zaidi ya ishirini kwa mche sasa piga hesabu eka moja inaweza accomodate miche 1000 na angalia bei ya tango mtaani kwenu ni ngapi. Bei ya shamba ni sh 300 so zidisha mara idadi ya tango kisha idadi ya miche urajua kwa mwezi unapata pesa ngapi maana mbegu hii ya monalisa ni ya mwezi

Hapa najibu swali la trojaan hapo juu
 
Mkuu inalipa si haba hata kwa bei hiyo ya shambani ni nzuri sana.
vipi kwenye nasafi ya upandaji baina ya mche na mche na umwagiliaji wake ni kama ule wa nyanya?
challenges zake kwenye wadudu zinakuwaje?
Ahsante.
 
Naamini utatoa maelekezo murua namna ya kufika hapo kwenye mafunzo badala ya kusema Kibaha tu! Si unajua Kibaha na ukubwa na pia utarajie wageni ambao hawaijui Kibaha KABISA. Asante.
kibaha kwa mathias, jamaa kaacha na namba za simu, mpigie kabla ya kwenda kwa ajili ya details
 
YAANI NIMEKUPENDA BURE...umenifurahisha..naufeel umuhimu wa JF
 
Mkuu inalipa si haba hata kwa bei hiyo ya shambani ni nzuri sana.
vipi kwenye nasafi ya upandaji baina ya mche na mche na umwagiliaji wake ni kama ule wa nyanya?
challenges zake kwenye wadudu zinakuwaje?
Ahsante.

Km unasimamisha miche utapandas kwa upana wa futi moja baina ya mche na mche ila km unaiacha inatambaa unapanda angalau mita 1 na umwagiliaji wak ni km kwa nyanya
 
Km unasimamisha miche utapandas kwa upana wa futi moja baina ya mche na mche ila km unaiacha inatambaa unapanda angalau mita 1 na umwagiliaji wak ni km kwa nyanya

Nashukuru sana mkuu kwa haya maarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…