Jamani acheni kutoa kejeli, kauli kam hizi zinaonyeshwa jinsi mnavyosahau mlikototoka na mlikopita, au hamkuwahi kupitia basi bahati yenu!!! lakini ndungu zangu nyie sikieni tuu kukaa mtaani kutafuta kazi, hizo frustrautations mhadithiwe!! ndo maana mnakurupuka kupost.
Kama kuna mtu aliye na info amsaidie!!! naomba kukushauri ndugu yangu huenda ni mwanzi wa kukufanya kuwa tajiri, ukaangalia uwezekano wa kuwa mjasiriamali, angalia side ya tourism industry inayokuwa vizuri uone ni wapi unweza kufit in!!! kama vipi piga hata tofali utachomoka tu ndugu yangu. Haya maajira wakati mwingine yanatulemaza sana!!! kubishana na mshahara kila mwisho wa mwezi, ucione watu wanafanya kazi za kuajiriwa wana raha waone tuu wanacheka wakiwa na wenzao wakiwa wenyewe mambo sio shwari!!!! tuangalie pia na uwezekano mwingine