Tours and travel business

Tours and travel business

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,188
Reaction score
6,244
Habari zenu wakuu. Nataka kuanzisha biashara ya tours and travel, naomba muongozo wa kusajili biashara tajwa. Natakiwa kupita wapi na wapi mpaka nikamilishe usajili na estimated cost ni ngap?

Ahsante
 
Wageni unao.........?.......au fafanua ni ktk nyanja gani coz hii sekta ni pana sana..............
 
Wageni unao.........?.......au fafanua ni ktk nyanja gani coz hii sekta ni pana sana..............

Hapana, nahitaji kusajili kwanza ili nitambulikane ndio niweze kufanya biashara hio. Maana nataka kudeal na mahoteli sasa wanahutaji kuona usajili..... Ndiocho nachotaka kwanza
 
Ukiachia TRA hakuna sehemu nyengine labda nayotakiwa kupita labda institute yoyote ile yenye kuhusika na biashara tajwa? Pia ni kiasi gani huko TRA watakuwa wanahitaji?

utahitaji kuonana na wizara ya utalii, kuna leseni flani ya kwao lazma uwe nayo
 
Habari zenu wakuu. Nataka kuanzisha biashara ya tours and travel, naomba muongozo wa kusajili biashara tajwa. Natakiwa kupita wapi na wapi mpaka nikamilishe usajili na estimated cost ni ngap?

Ahsante

Ushauri wangu baada ya kupata leseni:

Usikose kutumia tovuti za kitalii kujitangazia biashara yako. (Tripadvisor.com).

Tengeneza tovuti ya hoteli yako. Pokea malipo kwa credit card.

Ukitoa huduma nzuri, utapewa "positive reviews. Review ni kitu cha kwanza naangalia kabla ya kufanya booking ya hoteli. Wageni wakiiponda huduma, sinunui.

Chagua nchi zinazofanya Biashara za utangazaji wa Utalii kama Ujerumani au Tokyo na jiunge nao. Tokyo kila mwaka nchi zaidi ya 80 zinakuja kutangaza biashara za Utalii wa nchi zao. (Tokyo Big Site)
 
Mi kwako ni Swali moja tu?
Umesomea fani hii?

Hapo ndio ningeanza kukushauri,maana wengi sana wanataka kuanzisha hii biashara wakiona kwamba wageni ni rahisi sana kuwapata.Maana maelezo yako ya hapo juu yananitia mashaka saaana.

Ila kwa ufupi andaa Capital ya pesa si chini ya 100m
 
Mim najua wakati wa usajili wa biashara yeyote kuna mambo ya TRA na Brela kwa tours sina idea nayo ila kwa biashara kama kampuni ya mambo ya IT lazima upite uko kote
 
Wazo zuri ndugu ila kama alivyosema ndugu hapo juu lazima Wizara ya utalii na maliasili napo upite mana nao wana vibali vyao huwa wana vitoa... kingine kama mtaji wako mdogo una weza ukaanza na travel agency mana yenyewe haichukui mtaji mkubwa sana kama tour operator tatizo watu wanachanganya tour na travel agency ni vitu viwili tofauti japo vyote vina weza kufanya kazi kwa pamoja... tour huwa wana base katika kuandaa safari za watalii na kuwapeleka katika vivutio vya utalii... wakati travel agency yeye kazi yake kuchukua tour package.. kutoka kwa mzalishaji ambaye huweza kuwa tour operator au tourist hotel na kwenda kuziuza... pia kwa final consumer ambapo hulipwa kwa commission au kwa top up.. katika hiyo product anayo uza so travel agency kama una mtaji mdogo nazani n bora kuanza nayo kuliko tour operator... ila kama upo vzr unaweza uka anza navyo vyote
 
Back
Top Bottom