Toxic people

geniusMe

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
1,311
Reaction score
1,780
Jamani naomba kuuliza namna gani unaweza kushugulika na toxic people, toxic people ni watu ambao mnaweza kuwa mnafahamiana sana kwa karibu au kidogo lakini huwa wanakufanyia vitu fulani vidogo vidogo ambavyo ukitafakari vibaya unaweza kuona wewe ndio mwenye shida labda ukajiwekea mashaka mwenyewe kwa jambo ambalo wala halina msingi

Mfano umeweka akiba yako umenunua gari lako safi una enjoy unamsikia rafiki yako wa karibu mpo kwenye group anasema watu tunapiga kazi bwana tupate pesa tujenge sio vijana wa siku hizi wanakimbilia kununua magari, anasema hivi makusudi akijua kwamba kwenye kundi hilo ni wewe tu umenunua gari wengine hawana, unajua kabisa hili ni dongo limetumwa kwangu indirect.

Unajiuliza lakini mbona anayesema hivi ni rafiki wa karibu mtu unayemthamini na kumuheshimu unajiuliza je mimi ndio sina akili au ni wivu wake? alafu baada ya miezi kadhaa unamuona jamaa amenunua gari na yeye wala hajaenda kujenga nyumba kama alivyosema.

Je, kauli gani toxic ambayo umewahi kuambiwa au kusikia ikiwa inasemwa makusudi ili kukufanya ujiwekee mashaka katika mambo yako binafsi?
 
Kuna demu mmoja marafiki zake walikiwa wanapiga stori
eti pisi kali wanaishiwa kuchezewa tu, sisi na sura zetu hizi ndoa zipo nnje nnje mwenzao ni kisu na alikuwa ndio ameingia kwenye mahusiano kwa muda huo [emoji3]
 
Usisikilize ya mtu fanya yako daima songa mbele usigeuke nyuma kaa na watu wenye ndoto kama zako mheshimiwa
 
Siku hizi hata hatusalimii amajifanya yupo busy na kazi atafukuzwa tu
Binadamu ni toxic +

...hapo hatujazungumzia ulozi,mijitu inataka mtu aishi kama watakavyo wao.
 
..chuki + wivu vitawamaliza watu sana,mimi kuna lishenzi flani lilijifanya kujenga uhusiano wa karibu na mimi kumbe jamaa ni chawi balaa

Sasa niliumia mkono akawa amenipaka dawa yake flani hivi....isee kumbe ile dawa nahisi ni ya kimizimu maana baada ya miezi kadhaa nilianza kuota mandoto ya hovyo,lengo lake lilikuwa ni kunipiga gonjwa isee.

..saiv ni wiki inaisha nimeporomoaha maombi,naona amebadilisha na njia.

...lilitaka kunitoa kafara pumbavu hili
 
Miaka 2005 kwenda mbele kumeibuka wimbi la wanaume kuwa na tabia za kike.
Unakuta mwanaume mwenzako ni mbeya,mchonganishi,wivu mwingi na vyote siku hizi alivonavo mwanamke yeye ndio mfanyaji.
Kuanzia maofisini,majumbani mpaka vijiweni
 
Ignore/mpotezee hata kama mpo sehemu moja ya kazi.Utaishi kwa raha sn.
 
Mkuu mpaka mtu anaongea hivyo ngumi unakuwa umeziacha wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…