geniusMe
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 1,311
- 1,780
Jamani naomba kuuliza namna gani unaweza kushugulika na toxic people, toxic people ni watu ambao mnaweza kuwa mnafahamiana sana kwa karibu au kidogo lakini huwa wanakufanyia vitu fulani vidogo vidogo ambavyo ukitafakari vibaya unaweza kuona wewe ndio mwenye shida labda ukajiwekea mashaka mwenyewe kwa jambo ambalo wala halina msingi
Mfano umeweka akiba yako umenunua gari lako safi una enjoy unamsikia rafiki yako wa karibu mpo kwenye group anasema watu tunapiga kazi bwana tupate pesa tujenge sio vijana wa siku hizi wanakimbilia kununua magari, anasema hivi makusudi akijua kwamba kwenye kundi hilo ni wewe tu umenunua gari wengine hawana, unajua kabisa hili ni dongo limetumwa kwangu indirect.
Unajiuliza lakini mbona anayesema hivi ni rafiki wa karibu mtu unayemthamini na kumuheshimu unajiuliza je mimi ndio sina akili au ni wivu wake? alafu baada ya miezi kadhaa unamuona jamaa amenunua gari na yeye wala hajaenda kujenga nyumba kama alivyosema.
Je, kauli gani toxic ambayo umewahi kuambiwa au kusikia ikiwa inasemwa makusudi ili kukufanya ujiwekee mashaka katika mambo yako binafsi?