Toyo 150 vs Boxer bm 150

Agera 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
4,088
Reaction score
4,226
naombeni msaada wa piki piki hizi mbili kati ya toyo 150 na boxer bm 150 , mimi ni mpenzi sana wa piki piki toka india kama hyo boxer nataka nunua kwa ajil ya mbishe zangu za mjin na mara moja moja kuifanya boda boda ,ila kuna ndugu yangu mmoja yeye ana toyo kwa sasa inaenda mwaka wa tatu anaijal service kila wiki mbil na akaniambia bora toyo asikwambie mtu mara akaanza niambia kuwa spea za boxer bei ghal mfano cha kubadil gia ni elfu 70 wakat cha toyo buku 8 mara tair ni laki wakat la toyo elfu 70 na vitu vingne cha mwisho akaniambia boxer ikichoka huez uza na ukiuza labda milion wakat toyo ata ikichoka ukipga service ya laki unauza robo tatu ya bei ulionunulia .MSAADA TAFADHAL WENY UFAHAM ZAID
 
Boxer nimetumia katibia miaka mitano haikuwahi kunisumbua niliiuza kwa 1.2m nimenunua nyingine INA mwaka na ukiiona ni kama mpya watu wengi hawajui boxer ni Pikipiki nzuri kikubwa ijali kwenye service na tumia oil ya BP kumbuka pia kubadili oil filter sasa wengi oil filter hawabadilishi na oil wanayoitumia haieleweki eleweki na boxer ni kama kitu chochote cha moto ukiona tatizo rekebisha na usitake kuweka Speir fake
 
kwa mfano hyo oil filter inaweza kuwa bei gani sababu me ninachoogopa ni gharama tu
 
Boxer ni Mashine hatari, mchina haoni ndani. Kuna pikipiki nyingine Nzuri kuliko Boxer, Honda Ace. Hiyo hata Boxer cha mtoto. Ni ngumu mno, imara na inanusa mafuta, hailambi. Hizi bei yake ipo sawa na boxer na spea ni ghali kama boxer ila uimara na comfortability ni zaidi y Boxer.

Nime zitumia zote Boxer 150 na Honda Ace ila Honda ndio chuma zaidi, Hapo ni Mhindi dhidi ja Mjapani.
 
Oil filter elf 6 tuu na hubadilishi frequently acha uoga kijana boxer matunzo km kutunza muoga kweli shida usinunue mwaka huitaman lkn cheza na oil na spare original utaipendaa hii mashine hataree
 
kumbe honda ace bei ni sawa na boxer
 
mweny picha ya honda hyo aweke niione
 
BP oil 15 oil filter 5
Fundi mpe 5 akuchekia na vitu vingine vya kuajast ajast muda gani tena wa kufanya service ni matumizi yako tu kwa kawaida Pikipiki inatakiwa kufanyiwa service kila baada ya kilomita 1000 kama mie unafanya Mara moja kwa mwezi na Pikipiki boxer natumia ni kwa ajili ya kwenda job na kurudi tu
 
kayenga oil unabadilisha baada ya mda gan?
 
Boxer ni nzuri sana ukiitunza na usipofanyia biashara baaasi utaipenda sana
Fanyia matengenezo usigongwe gogwe
 
Boxer watu wengi hawazipendi kwa sababu huwezi kubebea mizigo mizito km ilivo Toyo. Toyo inavumilia mizigo mizito, lakini boxer ni za luxury za town, na safari coz ni nyepesi haili mafuta na ina spidi nzuri.
 
Ila hizi boxer zinazoingia sokoni sasa hivi usijaribu mkuu, najuuuuutaa.
 
Alafu tank lna neno boxer maandish mekundu zle ctak ata kuzickia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…