Toyota Allion Vs Toyota Premio ZZT 1.8L

Toyota Allion Vs Toyota Premio ZZT 1.8L

Habari wakuu zangu!

Mimi ni kijana nimekuwa nikitamani kumiliki ka usafiri, Tamanio langu ilikuwa ni kumiliki Toyota Premio 2005 ZZT 1.8L yenye taaa tofauti na zile model za 2001-2004 .
Sasa nimejipapasa nimepata budget kama 13mil
Nimejaribu kutafuta premio yenye vigezo hivyo imekuwa Changamoto ila nimepita kwenye website ya SBI Motors japan nikaiona Toyota Allion 2003 ZZT 1.8 L ina milleage chache almost 24,000 km na ina hali nzuri sana na iko kwenye budget hiyo.

Ombi langu kwenu naomba ushauri wenu kati ya gari hizo mbili, Je niongezee budget nipate premio ya 2005 ambayo almost ni kama 16.5 mil au nichukue hiyo Allion 2003 yenye hali nzuri na milleage chache?

Je Fuel Consumption ,matengenezo na Spare parts kati ya hizo aina mbili za magari ukoje?

Naombeni ushauri wakuu wangu!

Nashukuru

Allion naona iko pouwa tena ile A18 hatari sana
 
Kapotea jamaa...pengine bado ipo bandarini TRA wanaihesabia tu
 
Mkuuu mrejesho? Vp gari ilifika? Unaionaje?

Habari mkuu
Mzigo ulifika ndani ya siku 35 around mwezi wa NANE mwishoni 2021.
na sikukuu za xmass na mwaka mpya imeenda Bukoba na kurudi.

Ahsanteni wakuu kwa msaada wa mawazo.
IMG_4489.jpg

IMG_4490.jpg

IMG_4487.jpg
 
Hata allion pia mkuu ni gari kali sana. Nimeitumia iko vizuri, tofaut yake na hyo nyingine ni miaka tu. Ila premio na allion ni jamii moja na zote zinatumia mafuta vizuri sana/ ni economy.
Mi yangu ni ya 2004.
0655362575
Mkuu cc ngapi yako hiyooo Alion na mafuta inatumiaje na bei yake ni shilingi ngapi ina range
 
Mkuu cc ngapi yako hiyooo Alion na mafuta inatumiaje na bei yake ni shilingi ngapi ina range

Wakuu pole!
Nachelewa kuona Message App hainipi notifications.

Hii Ni Cc 1790 mimi naona ulaji wa Mafuta Ni mzuri
Nikiweka full tank nadunda nalo 3weeks Sema mimi siyo mzuriraji.
Kwenda job na kurudi takribani 15 km per day. Plus kuzurura mara moja moja.

Mfano nilisafiri nalo Dsm to Bukoba nilitumia full tank mbili Ila mafuta yakabaki .
Tank ya kwanza nilitoka Dsm mpaka Nzega.
 
Uliagiza mwenyewe au ulitumia agent?

Niliagiza Mwenyewe kaka.
Ma agent bei ziko juu.
Assume mimi nilagiza mwezi wa nane mwaka Jana budget ilikuwa 13.5Mil bila BIMA.

Nililipia mwenyewe Bank na document nikatumiwa via DHL nikamtafuta jamaaa wa Clearing akanitolea gari. Nilimpa kama 250,000 hivi
Gharama za TBS na Bandari zote nililipa mwenyewe kwa Control number.
IMG_4367.jpg

IMG_4365.jpg
 
Niliagiza Mwenyewe kaka.
Ma agent bei ziko juu.
Assume mimi nilagiza mwezi wa nane mwaka Jana budget ilikuwa 13.5Mil bila BIMA.

Nililipia mwenyewe Bank na document nikatumiwa via DHL nikamtafuta jamaaa wa Clearing akanitolea gari. Nilimpa kama 250,000 hivi
Gharama za TBS na Bandari zote nililipa mwenyewe kwa Control number.View attachment 2166462
View attachment 2166463
Hongera mkuu

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom