Toyota Alphard: Ubora na Mapungufu yake

Toyota Alphard: Ubora na Mapungufu yake

Fereke

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
297
Reaction score
846
Ndugu wadau naomba kwa wale wenye uelewa juu ya aina hii ya magari, ubora wake, matumizi ya mafuta, na chochote kizuri kuhusiana na magari haya.

Pia naomba kujua mapungufu yake kwa wale wenye uzoefu nayo.

Je, kuna utofauti gani kati ya Toyota alphard "V" na Alphard "G" ingawa kwa macho huwa naona kama G ipo juu kidogo but wazoefu nadhani watanisaidia.

Natanguliza shukrani.

NB: hata kama mtu anaiuza ningependa kujua bei na taarifa zake nyingine muhimu.

1608716902154.png

Toyota Alphard
 
hiyo gari ya kibabe sana uwezi fananisha na kina noah, engine iko poa sana nguvu ya kutosha pia sunspension iko vyema sana, mafuta ni kama 12km /l highway na mjini ni around 9.5-10km / L
Mkuu nashukuru sana kwa uzoefu uliotoa, ingawa ningetamani kujua utofauti wa Alphard V na Alphard G kama unafahamu ili nifanye maamuzi sahihi.
 
My favourite japanese family car..

Hizi zipo 3 generation sasa sijui unaongelea ipi

Kuna model of 2002-07
Kuna model of 2008-15
Kuna model of 2015-

Hapo nahisi utakuwa unaongelea 1st generation ambayo inakuja kwa machaguo ya engine mbili

2.4 L 2AZ-FE I4
3.0 L 1MZ-FE V6

Nakushauri uchukue hyo ya 2.4 kwa ajili ya economy maana sioni maana ya kuchukua 3.0 V6 who needs speed and power in a family car? u get my point i think

Strength
-Space
-Power
-Comfortability
-Handling
-Economy fuel consumption for a car of its size
-Technology...automatic doors...back camera...media settings on stearing wheel..parking sensor..distance sensor etc

Weakness
-Low ground clearance
-Soft bumpers material

conclusion
ichukue tu hyo gari ila itunze itadumu

-hyo ya 2002-2008 utaipata kwanzia 15ml -20ml

-hyo ya 2009-15 imechangamka kidogo bei yake

-hyo ya 2015- ni bad news bei yake inaanzia 70 milion huko na zinapatikana za 0 km na used pia
 
my favourite japanese family car..

hizi zipo 3 generation sasa sijui unaongelea ipi...
Asante sana mkuu umenifungua macho kwa mengi ninaihitaji sana hiyo gari ila sikua naijua kwa undani that's why nikasema nachojua zipo zilizoandikwa Alphard G na Alphard V sijui zaidi.

Hiyo bei 2002-2008ambayo umesema ni 15-20m ni kwa kuchukua kwa mtu,au show room maana mie ningepata hata kwa mtu ikiwa nzima poa tuu najua kuagiza ni gharama zaidi na mfuko wangu haufiki huko.
 
Asante sana mkuu umenifungua macho kwa mengi ninaihitaji sana hiyo gari ila sikua naijua kwa undani that's why nikasema nachojua zipo zilizoandikwa Alphard G na Alphard V sijui zaidi...


Hiyo bei 2002-2008ambayo umesema ni 15-20m ni kwa kuchukua kwa mtu,au show room maana mie ningepata hata kwa mtu ikiwa nzima poa tuu najua kuagiza ni gharama zaidi na mfuko wangu haufiki huko.

kwa mtu unapata kuanzia 12-15 maana mwaka jana nilimsaidia mzee wangu kuagiza ilikuwa ya mwaka 2004 3.0 V6 CIF ilikuwa 3480$ na total import tax ilikuwa 7922065 tsh

so jumla hadi usajili ilicost
7,922,065+3,480×2,200
=15,578,065

kwahyo kama ukiona mtaani unatafuta alafu wote wanataka kwanzia milioni 14 bora uongeze moja au mbili uagize tu
 
Mkuu nashukuru sana kwa uzoefu uliotoa..ingawa ningetamani kujua utofauti wa Alphard V na Alphard G kama unafahamu ili nifanye maamuzi sahihi.
Mbona umetaja v na g tu m huijui au?
 
Asante sana mkuu umenifungua macho kwa mengi ninaihitaji sana hiyo gari ila sikua naijua kwa undani that's why nikasema nachojua zipo zilizoandikwa Alphard G na Alphard V sijui zaidi...
Hiyo bei 2002-2008ambayo umesema ni 15-20m ni kwa kuchukua kwa mtu,au show room maana mie ningepata hata kwa mtu ikiwa nzima poa tuu najua kuagiza ni gharama zaidi na mfuko wangu haufiki huko.
Kuagiza sio gharama mkuu,ni very cheap kama tu utasubiri kwa siku 45,bei yake inaanzia 15.6 mpaka 16.7 check me pm for more info.
 
Mimi ni mpenzi wa magari mazuri mazuri ninatafuta gari lenye uwezo wa kubeba watu 8, kuna haya yanayoitwa Alphard.

Ninapokuja kwenye kuchagua nakwama, bajeti yangu ni ndogo halafu nimeona kuna aina nyingi. Ninaomba mwenye uzoefu asaidie kunielezea tofauti ya Alphard G, Alphard Hybrid, Adalphard V, na Alphard yenyewe

alphad.PNG
 
Back
Top Bottom