Mie napenda utulivu wa inline 6, hivyo 1G naipa nafasi zaidi. Faida pia ya 1G ni upatikanaji wa spare parts. Ni engine common saana hapa kwetu. Maana imeanzia kwenye GX100 ya kina Mark 2, Chaser, Cresta, then kwenye GX110 Mark 2 na Verossa. Pia kuna Crown za kizamani zina 1G. So ni rahisi saana kuimaintain.
3S ya kwenye Altezza ni very unique. Ilitengenezwa kwa ajili ya Altezza pekee. Kumbuka kuna engines za 3S kibao mpaka kwenye Rav4, ila hiyo unayoiona kwenye Altezza ni ya Altezza pekee. So ikizingua kitu unaweza jikuta unasumbuka kukipata mpaka upate cha hiyo hiyo ya Altezza.
Kwa upande wa gharama ya turbocharger, inapishana saana kutokana na kit utakayochagua. Ila kama unataka kit nzuri, nafikiri kuanzia 5m. Mafundi wengi wapo Dsm na Arusha.