Toyota Brevis na heshima zake

Toyota Brevis na heshima zake

Yaani bila aibu unakuja kusifia toyota brevis? Uwe serious.unaona ni heshima kuwa na toyota brevis? Sasa na wenye magari nao waje waseme nini? Muwe serious...siyo mkinunua tu gari mnakuja kutupamba humu.na wenye magari wamenyamaza.

Unasifia toyota brevis na wamiliki wa BMW wamo, na wamiliki wa BENZ wamo humu, na wamiliki wa Range, Audi, Bentley, Escarade wamo wamenyamaza.
Jamaa si katoa mawazo yake sio lazima ukubalianenae, sasa mbona wew umeleta majina ya brand za magari tu apo, na sio magari halisia, mtu anaweza miliki Toyota brevis yenye ubora kuliko BMW, siku nyingine uwe ukitaka kufananisha uwe unakuwa specific kidogo,
 
gari isiyozidi 1.5 tonne kuwa na zaidi ya 180kph huwa hainiingii akilini (forget of its aerodynamics)
Una uhakika...???
Kuna corolla 110 kama sikosei hapa Arusha nimeiona kwa macho yangu ina 220 kph na injini ni 1.5 l...
kuna nissan pia nimeona injini 1.5 L lakini 220 kph....

Na hii corolla na hii Nissan zote zipo chini ya 1.5 ton..

Magari mengi ya Japan yaliyotengenezwa mahususi kwa soko la Ulaya kuwa na speed zaidi ya 200 ni swala la kawaida.

Japan kwa sheria zao mwisho ni 180kph.
 
Nimeendesha gari nyingi.
Brevis tunayo nyumbani, Kiufupi ni gari Nzuri sana ndani hata muonekano wa Nje, Inachanganya sana Haraka, Ni nyepesi, Mashimo inawez kupiga na ndani husisikie.

CHANGAMOTO ZAKE.
1. Spea zake ni ghali.
2. Inakula sana mafuta.
3. Dhaifu kwenye Mchanga au tope, ni rahisi sana kunasa hasa ikiwa nyepesei ila ikiwa na watu au imejaa Pulling yake ya Kuchanganya haraka inaisaidia.
Ila hakuna kizuri kisicho na Gharama.
 
Brevis sio poa, ilichotufanyia kweny harusi ya ndugu yangu dah. Gar ilichukuliwa temeke tukaiwekea mafuta ya bukuten, ikafika tandika kumchukua baba harusi kuelekea safar ya kitunda. Ile tunafika buza ikawekewa mafuta mengne ya bukuten, tukafika kitunda tukaoa then tukageuza, ile bwana na bibi harus wanashuka tu, tunaambiwa haiwezi kutoka mafuta yamekata... Kila mtu anashangaa yameishaje...
Brevis inataka full tank, au walau nusu tank.
 
altezza engine yake ni cc1980 wakati brevis ni cc2400-3000, ulaji wake kwa cc 2400 ni sawa na mark x na crown athlete kwa cc 3000 ni zaidi.
Ulaji wa altezza wa kawaida sana haufiki hata kwa Subaru forester
Altteza ipi unaisemea hapa ya 1G-Fe au 3s-ge?
 
Back
Top Bottom