Toyota Brevis na heshima zake

Jamaa si katoa mawazo yake sio lazima ukubalianenae, sasa mbona wew umeleta majina ya brand za magari tu apo, na sio magari halisia, mtu anaweza miliki Toyota brevis yenye ubora kuliko BMW, siku nyingine uwe ukitaka kufananisha uwe unakuwa specific kidogo,
 
gari isiyozidi 1.5 tonne kuwa na zaidi ya 180kph huwa hainiingii akilini (forget of its aerodynamics)
Una uhakika...???
Kuna corolla 110 kama sikosei hapa Arusha nimeiona kwa macho yangu ina 220 kph na injini ni 1.5 l...
kuna nissan pia nimeona injini 1.5 L lakini 220 kph....

Na hii corolla na hii Nissan zote zipo chini ya 1.5 ton..

Magari mengi ya Japan yaliyotengenezwa mahususi kwa soko la Ulaya kuwa na speed zaidi ya 200 ni swala la kawaida.

Japan kwa sheria zao mwisho ni 180kph.
 
Nimeendesha gari nyingi.
Brevis tunayo nyumbani, Kiufupi ni gari Nzuri sana ndani hata muonekano wa Nje, Inachanganya sana Haraka, Ni nyepesi, Mashimo inawez kupiga na ndani husisikie.

CHANGAMOTO ZAKE.
1. Spea zake ni ghali.
2. Inakula sana mafuta.
3. Dhaifu kwenye Mchanga au tope, ni rahisi sana kunasa hasa ikiwa nyepesei ila ikiwa na watu au imejaa Pulling yake ya Kuchanganya haraka inaisaidia.
Ila hakuna kizuri kisicho na Gharama.
 
Brevis inataka full tank, au walau nusu tank.
 
altezza engine yake ni cc1980 wakati brevis ni cc2400-3000, ulaji wake kwa cc 2400 ni sawa na mark x na crown athlete kwa cc 3000 ni zaidi.
Ulaji wa altezza wa kawaida sana haufiki hata kwa Subaru forester
Altteza ipi unaisemea hapa ya 1G-Fe au 3s-ge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…